P5 TANZANIA INAKULETEA WASIFU WA WAGOMBEA KITI CHA URAIS WA TANZANIA,TUNAANZA NDANI YA UKAWA,Mh.Edward Lowassa
Edward
Ngoyai Lowassa
|
|
Mbunge
|
|
Bunge la
|
|
Jimbo la uchaguzi
|
Monduli (Arusha)
|
Tarehe ya kuzaliwa
|
26 Agosti 1953
|
Chama
|
CHADEMA (tangu 28/07/15)
|
Tar. ya kuingia bunge
|
tangu 1990
|
Alirudishwa mwaka
|
2005
|
Alingia ofisini
|
2005
|
Alitanguliwa na
|
|
Dini
|
Mkristo
|
Elimu yake
|
Chuo Kikuu
|
Digrii anazoshika
|
MA (Development Studies)
University of Bath (Uing.)
|
Kazi
|
mwanasiasa
|
Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953)
ni mwanasiasa
nchini Tanzania.
Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hiyo tarehe 30 Desemba 2005
akajiuzulu tarehe 7 Februari 2008
kwa kutajwa katika kamati ya bunge ya uchunguzi katika utoaji wa tenda kwa kampuni
ya umeme ya Richmond kutokana na uzembe wa watendaji walio chini yake.
Lowassa ni mwenyeji na alikuwa mbunge
wa Monduli
katika Mkoa wa Arusha.
Alisoma shahada ya kwanza katika mada ya tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii kwenye Chuo
Kikuu cha Hull nchini (Uingereza).
Mnamo tarehe 28 Julai 2015
alijunga rasmi na chama
cha upinzani cha CHADEMA. Hiyo ni baada ya
kukatwa jina lake katika kinyang'anyiro cha Urais kupitia chama tawala
cha Chama cha Mapinduzi.
Yaliyomo
- 1 Nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika
- 1.1 Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (2005 - 2008)
- 1.2 Waziri wa Maji na Mifugo (2000 - 2005)
- 1.3 Waziri wa ardhi na makazi (1993 - 1995)
- 1.4 Nyadhifa nyinginezo
- 2 Uchaguzi mkuu 1995
- 3 Viungo vya nje
Nyadhifa
mbalimbali alizowahi kushika
Lowassa ni mwanasiasa
mkongwe mwenye uzoefu mbalimbali katika siasa
za nchini Tanzania. Lowassa amewahi kushika vyeo mbalimbali katika serikali ya Tanzania kama vile:
Waziri mkuu wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (2005 - 2008)
Tarehe 29 Desemba 2005 Lowassa
aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya
kuthibitishwa na bunge na kula kiapo, mchakamchaka
wa kuwaletea Watanzania maendeleo
ukaanza. Nidhamu,
utiifu na uwajibikaji
vikaongezeka miongoni mwa watumishi
wa umma na viongozi waandamizi, serikali ukarudisha sura yake ya
serikali maana viongozi waandamizi wakiwemo mawaziri
walijua yupo mtu makini na jasiri wa kuuliza juu ya uwajibikaji wao.
Kazi ya kuboresha shughuli za maendeleo
ya jamii zikaanza, moja kubwa ikiwa ni kuhakikisha
kila mtoto mwenye umri wa kuanza elimu ya msingi anapatiwa
nafasi na kila aliyefaulu kwenda sekondari
pia kupatiwa nafasi. Anasifiwa kwa kusimamia kikamilifu kazi ya kuhimiza ujenzi
wa sekondari za Kata na nyumba za walimu nchini Tanzania.
Serikali ya awamu ya nne ilianza kwa
mitihani mikubwa matatu, wa kwanza ulikuwa na upungufu mkubwa wa chakula ulioikumba baadhi ya mikoa na
kutishia maisha ya wananchi, wa pili ulikuwa ni wimbi kubwa la kutumia silaha hasa kwenye mabenki na wa tatu
ni upungufu mkubwa wa uzalishaji wa umeme
uliotokana na kushuka kwa kiasi kikubwa cha maji katika bwawa la mtera na
kutishia nchi kuingia gizani.
Waziri Mkuu Mhe Lowassa akiwa msimamizi
mkuu wa kazi za serikali na mwenyekiti wa kamati ya kushughulikia maafa
alimuhakikishia Raisi kwamba pamoja na kuwepo tatizo la upungufui mkubwa wa
chakula hakuna mtanzania atakayekufa kwa njaa, Uthibitisho huo wa Waziri Mkuu
ukampa nguvu kiongozi wa nchi Raisi wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania kulitangazia taifa kuwa hakuna atakayekufa kwa njaa. Mhe
Lowassa alisimamia kazi ya kutafuta chakula kile kona ya nchi yetu na nje ya
nchi na kukipeleka sehemu zenye mapungufu hadi hali ilipokuwa shwari. Sambamba
na kukabili upungufu wa chakula katika ushiriki na ushauri wa karibu wa waziri
Mkuu kuhusu masuala ya usalama serikali iliweza kudhibiti wimbi kubwa la
ujambazi liliokuwa limezuka.
Hatua muhimu iliyochukuliwa na Serikali
katika kukabili tatizo la upungufu wa nishati ya umeme ilikuwa ni kuchukua hatua za
haraka kupitia Tanesco kutangaza na kupata mzabuni wa kuzalisha umeme wa
dharura ili kuokoa tishio la nchi kuingia gizani. Baada ya Tanesco kupitisha
zabuni ya kampuni ya Kimarekani na baada ya kampuni hiyo kushindwa kufanya kazi
na kuhamishia mkataba wake kwa kampuni ya DOWANS hapo ndipo sinema ya kisiasa
ilipoanza.
Sinema ya Richmond ambayo imekuwa
ikijulikana kama sakata la Richmond ilianzia katika kuunda kwa tume ya
kuchunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura, tume hiyo ilidai
kampuni ya Richmond ilianza katika kuunda kwa tume ya kuchunguza mchakato
wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura, Tume hiyo ilidai kampuni ya Richmond
ilikuwa ni kampuni ya mfukoni, jambo ambalo inawezekana lina ukweli maana hata
kabla ya tume kuundwa Waziri Mkuu Edward Lowassa alipata shaka na kampuni
hiyo pale iliposuasua kutekeleza mradi na akawa ameshauri mkataba na kampuni
hiyo uvunjwe lakini ushauri wa mtaalamu na wanasheria ulitaka serikali
ivumilie.
Tume ilidai viongozi wa serikali wa
wizara husika na Waziri Mkuu walikuwa wakihimiza Tanesco kukamilisha mchakato
wa kumpata mzabuni haraka, jambo ambalo hakikuwakosha maana ni jamba ambalo
lilikuwa kwenye mujibu wao kuona nchi haiingii gizani kwa manufaa ya kiuchumi
na kiusalama. Pia ni vyema ieleweke pia kwa umuhimu wa umeme kiuchumi na
kiusalama suala la kupata mitambo ya kufua umeme wa dharura lililozungumzwa na
kupata vikao vyote muhimu vya serikali ngazi ya Taifa likiwemo baraza la
mawaziri.
Sinema zaidi ya kisiasa ilikuja
kubainika katika mambo makubwa matatu; Kwanza ni kumtaka Waziri Mkuu apime na
anatakiwa kuwajibika katika jambo ambalo halibainishi kosa lolote kwake,
kiutawala wala kisiasa. Mbili mabishano ya wanasiasa juu ya kutumia au
kutoendelea kutumia mitambo ya DOWANS, na tatu mabishano ya wanasiasa juu ya
kulipwa au kutolipwa kwa kampuni ya DOWANS.
Ili kulinda heshima ya serikali nzima,
Chama tawala CCM na pia ili kuepuka mgawanyiko miongoni mwa
wanachama, wananchi na viongozi Lowassa aliamua kujiuzulu nafasi ya Waziri
Mkuu. Wabunge wa CCM waliokutana kama kamati kuzungumza suala hili zaidi ya
asilimia 80% walitaka Waziri Mkuu Lowassa asijiuzulu kwa kuwa hausiki na
chochote. Na kwa upande wa kamati ya bunge, mwenyekiti wa kamati hiyo Harrison
Mwakyembe, mnamo tarehe 15 February 2008 alikiri kuwa, Edward Lowassa
alijiuzuru kwa makosa ya watendaji wa chini yake.
Kuhusu hoja ya kulipwa DOWANS na
kuendelea kutumika kwa mitambo ambayo ililetwa na DOWANS jambo hili lilikwenda
kwenye mabaraza ya kimataifa na kuonekana wana haki ya kulipwa na
mitambo iliyodaiwa na wanasiasa kuwa haifai ndiyo inayoendelea mpaka leo
kufua umeme na Raisi ya Marekani Baraka Obama katika ziara yake hapa nchini
aliitembelea na kusema ni moja ya mitambo bora sana katika bara la Afrika, lakini
kwa wanasiasa bado sinema bado inaendelea.
Waziri wa Maji
na Mifugo (2000 - 2005)
Mwaka 2000 – 2005 alikuwa waziri wa
maji na maendeleo ya mifugo. Mwanamapinduzi Edward Ngoyai Lowassa aliitumia
tena nafasi kutekeleza jukumu alilokuwa amepewa na taifa kwa kuweka na
kusimamia mikakati ya kuhakikisha maeneo ya vijiji vyetu vinapata maji kama
sera ya CCM ilivyoelekeza, Hata hivyo alikerwa na matatizo mawili makubwa, moja
lilikuwa ni kampuni ya iliyokuwa na imeingia mkataba na serikali kusambaza
huduma za maji (city water) kushindwa kutekeleza wajibu wake na la pili
lilikuwa ni tatizo la maji katika mkoa wa Shinyanga na baadhi ya mkoa wa
Mwanza.
Kwa kuwa Lowassa hana tabia ya
kulalamika wala kusikitika bali kuchukua hatua za kutafuta ufumbuzi,
Mwanamapinduzi huyu aliamua kufanya maamuzi magumu lakini muhimu kwa
kuvunja mkataba na city water, uamuzi ambao aliusimamia pamoja na kuwepo kwa
mikono ya watanzania wenzetu waliotaka city water waendelee kubaki ili wao
wanufaike. Uamuzi huu ulileta huzuni kwa watumiaji wa maji katika jiji la Dar
ingawa changamoto bado zipo hasa kutokana na ongezeko kubwa la watu na ujenzi
wa maeneo mapya katika jiji.
Zaidi ya hilo la city water waziri
Lowassa aliamua kuchukua hatua za kupanga na kuishawishi serikali kuingia
katika mradi mkubwa wa kutoa maji katika ziwa Victoria na kuyasambaza katika
mikoa ya Mwanza na Shinyanga, huu ni miongoni mwa miradi michache mikubwa
iliyotekelezwa kwa kodi za watanzania bila kutegemea ufadhili aidha pia ni
mradi uliowasaidi wananchi wengi katika maeneo bomba hili lilipopita na moja ya
manufaa makubwa ni kupungua kwa kwa magonjwa yaliyotokana na utumiaji wa maji
yasiyo salama.
Waziri wa ardhi
na makazi (1993 - 1995)
Akiwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya
Mijini, Lowassa alisimamia utekelezaji wa mkakati wa upimaji viwanja kwa
maendeleo ya miji na kupambana na tatizo lililokuwa limeanza kuota mizizi la
kuwagawia watu zaidi ya mmoja kiwanja kimoja.
Wale wakazi wa jiji hawatasahau uamuzi
mzito na mkubwa wa kufatia maamuzi ya Halmashauri ya jiji la Dar es
Salaam ya kumgawia mfanyabiashara mmoja eneo la uwanja wa kumbukumbu ya Uhutu
(Mnazi Mmoja) ili ajenge vibanda vya biashara. Uamuzi huu wa Mhe Waziri Lowassa
aliungwa mkono na vijana wanaofanya biashara mitaani (machinga) na wakaandamana
na kwenda kuvunja uzio wa mabati uliokuwa umewekwa na mfanya biashara huyo
katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Uamuzi huo wa Waziri
Lowassa ulizingatia kulinda heshima na hadhi ya Serikali na zaidi
ulizingatia kuwa matumizi ya viwanja vya mnazi mmoja ni kwa ajili ya shughuli
za umma na wananchi wanapaswa kuwa huru kuutumia na kuangalia shughuli
zinazofanyika bila kizuizi. Maamuzi ya aina hiyo hufanya na watu wenye uzalendo
na utaifa.
Nyadhifa
nyinginezo
- Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993)
- Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989 - 1990)
- Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhii ya umasini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
- Mbunge wa Monduli tangu 1990
Uchaguzi mkuu
1995
Mwaka 1995 Edward Lowassa aliamua
kuingia katika mchakato wa kumpata mgombea uraisi kwa tiketi ya CCM, Wakati huo
Lowassa aliombwa na Umoja wa Vijana kupitia kikao cha baraza kuu la Taifa
achukue fomu akiwa miongoni mwa wana CCM wanne ambao vijana waliamini wamaweza
kuliosaidia Taifa kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye maendeleo endelevu,
wengine waliokuwa waliokuwa wametajwa na Umoja wa vijana ni pamoja na Salim
Ahmed Salim, Laurance Gama na jaji mstaafu Mark Bomani.
Katika hatua ya kuchagua majina matatu
kati ya majina 11 yaliyoomba nafasi jiyo Lowassa akawa hakupendekezwa, lakini
hakununa wala kususa bali aliamini kuwa Mwanamapinduzi mwenzie Jakaya Mrisho
Kikwete ataweza kutekeleza dhamira aliyokuwa nayo ya kuwaletea watanzania
maendeleo, hivyo alirudi kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana wa CCM ambao
walihoji kwanini ameengeliwa na yeye kwa utii mkubwa kwa CCM aliwataka vijana
na viongozi wengine waheshimu maamuzi ya chama na kumuunga mkono Jakaya M
Kikwete. Ikumbukwe kuwa mwana-CCM mwingine aliyekuwa anakubalika kwa umma
Lowassa aliamua kuondoka mapema kuondoka CCM kwa sababu ndogo tu ya
kubadilishwa wizara na kuamua kwenda chama cha NCCR mageuzi ambako aligombea
uraisi kwa chama hicho na kuleta upinzani mkubwa.
Yapo maneno ya baadhi ya wanasiasa
kwamba kurtoteuliwa kugombea kwa Mhe Lowassa kulitokana na
kuonekana anamiliki fedha nyingi akiwa na muda mfupi kwenye utumishi
wa umma, lakini pia inasemekana kuwa wale waliohoji kukatwa kwa jina lake
kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya |Taifa majibu yalikuwa, CCM iliamua
kupeleka majina matatu kwenye mkutano mkuu ili wachague moja katika uwakilishi
huo wa majina walipenda apatikane mtu mzima mmoja, mwenye umri wa kati
mmoja na kijana mmoja, watu hao ni mzee David Msuya ambae ni mtu mzima, Benjamini
Mkapa ambae umri wake ulikuwa wa kati na kijana ambae ni Jakaya Kikwete.
Lakini maneno hayo ya baadhi ya
wanasiasa hayakuishia hapo wakadai baada ya Rasi Mkapa kuchaguliwa hakumteua
Mhe Lowassa kwa kuwa aliagizwa na Mwalimu Nyerere asimteue mpaka achunguzwe
kama uwezo kiasi wa fedha alionao untokana na mapato halali, siyo halali
asimteue. Mwaka 1997 Rais Mkapa akamteua Lowassa kuwa Waziri wa nchi ofisi ya
makamu wa Rais mazingira. Maneno hayo ya baadhi ya wanasiasa ni ya ukweli basi
uchaguzi ulifanyika na kuonekana mapato yake ni halali au vinginevyo unaweza
kusema ni hisia za kimazingira.
Comments