MGOGORO WA ARDHI MTAA WA NSEMULWA BADO MBICHI,MKURUGENZI ATOA JIBU BILA SULUHU
NA.Issack Gerald-Katavi
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
imesema haijapokea malalamiko ya wakazi wa mtaa wa Nsemulwa kutopimiwa viwanja
vyao na kutozwa kiwango kikubwa cha pesa tofauti na kilichopangwa kupitia
mikutano.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi
Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Suleiman Lukanga wakati akizungumza na Mpanda
Radio ili kujibu suala la mgogoro wa ardhi uliopo Mtaa wa Nsemulwa kati ya
Ofisi ya ardhi ya manispaa hiyo na wakazi wa mtaa huo.
Amesema kuwa viwanja vimekwishapimwa
ambapo majibu haya yanakinzana na madai ya wakazi hao wanaohitaji kupimiwa
viwanja.
Mgogoro wa viwanja kutopimwa na kutozwa
kiwango kikubwa cha pesa kwa wakazi wa mtaa wa Nsemulwa, limedumu kwa kipindi
cha miaka mitatu mfululizo bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu huku wakazi hao
wakishindwa kufanya shughuli za maendeleo.
Comments