WAKAZI MPANDA WANDELEA KUWA GIZANI UMEME KUKATIKA,VIWANDA VYAKOSA UMEME SHUGHULI ZASIMAMA KWA MWEZI SASA
NA.Issack Gerald
TATIZO la kukatika Umeme mara kwa
mara Mkoani Katavi limesababisha
kuzorota kwa biashara ya mchele, kutokana na kukwama kwa ukoboaji wa mpunga zao
linalotegemewa na wakazi wengi mkoani Katavi.
Wafanyabiashara wa Mchele pamoja na wamiliki
wa Mashine za Kukoboa mpunga wameiambia P5
TANZANIA kuwa, shughuli za ukoboaji wa Mpunga zimesimama kwa sababu ya
ukosefu wa nishati ya umeme na kusababisha kupunguza kipato chao.
Mpaka sasa mwezi mmoja unakadiriwa
kupita ikiwa Mkoa wa katavi unakabiliwa na
tatizo la kukatika kwa umeme.
Mchele ambao unakobolewa Mkoani
katavi husafilishwa kwenda mikoa mbali mbali
nchini Tanzania pamoja na nchi jirani za Rwanda na Burundi, na kukuza
kipato cha wafanyabiashara wa mchele.
Hata hivyo taarifa ambazo zimekuwa
zikitolewa na Meneja wa Tanesco Mpanda Bw. Chacha Nsiku zinasema kuwa kukatika
kwa umeme kunatokana na matengenezo ya mitambo ya kuzalisha umeme.
Comments