UNAMFAHAMU MAGUFULI NA MAISHA YAKE TANGU KUZALIWA HADI SIASA?ONGEZA CHAKULACHA UBONGO NA P5 TANZANIA
Mhandisi John Pombe Magufuli |
JOHN POMBE MAGUFULI
Magufuli ni Nani?
Lakini je Daktari John Magufuli ni Nani?
Mgombea wa urais wa chama cha CCM katika uchaguzi mkuu wa
mwaka wa 2015 Daktari John Pombe Joseph Magufuli ni mbunge wa jimbo la Chato
lililoko mkoa wa Geita na ni waziri wa ujenzi wa Tanzania.
Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.
Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi
akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.
Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na
shahada ya uzamivu ya kemia.
Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya
sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .
Alizaliwa Oktoba 1959
Mhandisi John Pombe Magufuli wakati akijiunga na ccm 1995 |
Alipohitimu, daktari
Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union
akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.
Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la
Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa
Miundombinu.
Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na
kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.
Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea
ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.
Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na
maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.
Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais
Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.
Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye
msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa
kisaisa.
Anatambulika kuwa Mchapa kazi
Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa
barabara na majengo thabiti.
Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa
kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.
Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Bwana John
Magufuli alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina
iliyokuwa inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.
Comments