UHAKIKI MAJINA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MANISPAA YA MPANDA WAKWAMA,MKURUGENZI KUTOA TAARIFA BAADA YA VIFAA KUAWASILISHWA
NA.Issack Gerald-KATAVI
ZOEZI la uhakiki wa taarifa katika
daftari la kudumu la mpiga kura limeelezwa kuchelewa kuanza katika Manispaa ya
Mpanda kutokana na kucheleweshwa kwa vifaa, zikiwemo mashine za BVR.
Akizungumza na Mpanda P5 TANZANIA Ofisini kwake Mkurugenzi wa
Manispaa ya Mpanda Bw. Suleiman Lukanga amesema anatarajia kutoa taarifa kwa waliojiandikisha
katika daftari la mpiga kura ili wakahakiki majina yao baada ya vifaa vyote
kuwasilishwa.
Aidha amesema kuwa zoezi la sasa siyo kwa
ajili ya ambao hawakujiandikisha awali wakati wa kuboresha daftari la kudumu la
mpiga kura,bali ni kwa ajili ya kusahihisha makosa yaliyojitokeza wakati wa
zoezi hilo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza
kuanza kwa zoezi la uhakiki wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura kwa
Mkoa wa katavi Agosti mosi mwaka huu
ambapo hata hivyo wakazi manispaa yam panda walikuwa wameanza kushikwa na
wasiwasi kutoana na kutoona majina yao katika vituo walivyojiandikisha.
Comments