WAKAZI NSEMULWA KUWASHTAKI MAAFISA ARDHI MANISPAA YA MPANDA KWA WAZIRI WA ARDHI WAKIPINGA USUMBUFU UPIMAJI WA VIWANJA
NA.Issack Gerald-KATAVI
WAKAZI wa mtaa wa Nsemulwa Kata ya
Nsemulwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamekusudia kumuita Waziri wa Ardhi
nyumba na maendeleo ya makazi kutatua migogoro ya ardhi, wakiwatuhumu maafisa
ardhi Wilayani Mpanda kushindwa kutatua migogoro hiyo kwa miaka mitatu sasa.
Wakizungumza na Mpanda Radio, wakazi
hao zaidi ya elfu moja wamesema kuwa wamechoshwa na usumbufu wanaoupata kutoka
Ofisi ya Ardhi Wilayani, baada ya kutakiwa kutoa kiwango cha pesa kilicho nje
ya uwezo wao tofauti na kiasi walichoambiwa awali.
Aidha wamesema kuwa hawako tayari
kuhama kupisha wawekezaji na badala yake Ofisi ya ardhi ibatilishe tangazo la
kuwataka wakazi hao kuhama eneo hilo, ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.
Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda, Bw.
Suleiman Lukanga ameahidi kufuatilia suala hilo na kutoa majibu leo.
Ofisi za idara ya ardhi Katika
Manispaa ya Mpanda siyo mara ya kwanza kutuhumiwa kwa kuchelewesha utatuzi wa
migogoro ya ardhi bali malalamiko yamekuwa yakitokea katika maeneo mara kwa
mara.
Comments