JESHI LA POLISI KATAVI LASISITIZA KUTUNZA SIRI ZA RAIA WEMA KUPAMBANA NA UHARIFU
Na.Issack
Gerald-KATAVI
JESHI
la Polisi Mkoani Katavi limesema linaendelea na utaratibu wa kutunza siri za
raia wema wanaoshirikiana na Polisi kuwafichua waharifu wanaopelekea
kusababisha madhara kwa wananchi.
Hayo
yameelezwa leo na Afisa mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoani Katavi Focus Malengo
wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu ushirikiano kati ya jeshi la polisi
na raia katika juhudi za kupambana na
uharifu.
Aidha
amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi kata,na viongozi wa kata na
vijiji ili kuzuia uharifu kabla ya kutokea.
Miongoni
mwa uharifu ambao umekuwa ukitajwa mara kwa mara kutokea Mkoani Katavi ni
pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha.
Comments