20,162 KATI YA 22,596 WAJIANDIKISHA DAFTARI LA MPIGA KURA MAKAZI MAPYA YA KATUMBA
WANANCHI
20,162 kati ya 22,596 sawa na asilimia 89 ya wakazi wapya, Wilayani Nsimbo
Mkoani Katavi wamejiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Takwimu
hizo zimetolewa na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw. Hamis
Mnubi wakati akizungumza na Mpanda redio fm kwa njia ya simu.
Bw.
Mnubi amefafanua sababu ya kutofikia lengo la uandikishaji kuwa baadhi ya
wananchi wa makazi mapya walijiandika kwenye
kata zilizohusika katika zoezi la awali.
Zoezi
hili limezihusisha kata za Katumba, Kanoge, na baadhi ya vijiji vya kata za
Mtapenda na Litapunga.
Comments