MATUKIO YA WIKI KATAVI NA KWINGINEKO KUANZIA JANUARI 11 – 16,2016 NA P5 TANZANIA MEDIA



Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, January 12, 2016

Na.Issack Gerald-Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nzuri Ndizu (44) mkazi wa kijiji cha mbede anashikiliwa  na Jeshi la Polisi akiwa na meno 08 ya tembo vyenye uzito wa kg 50 ikiwa na thamani ya Tshs 120,000,000/= ambapo ni sawa na tembo 4 waliouawa kinume cha sheria.

Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,Kamanda wa polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo mnamo tarehe 08.01.2016 majira ya saa 3 na nusu usiku kwenye pori la akiba la Lwafe Wilayani Mlele Mkoani Katavi.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa,Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa katika pori la akiba la Lwafe kuwa kuna watu wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na kuanza kufuatilia taarifa hizo na hatimaye kumkamata mtuhumiwa Nzuri Ndizu  akiwa na vielelezo hivyo vilivyokuwa vimefichwa porini kusubili wateja.
Hata hivyo jeshi la polisi linaendela na uchunguzi zaidi
kubaini mitandao yote inayojihusisha na biashara hivyo haramu ya meno ya tembo ambapo mtuhumiwa atafikishwa afikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Posted By:Issack Gerald | At:Monday, January 11, 2016

Na.Issack Gerald-Mpanda,Katavi
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.William Tate Ole Nasha,amemwagiza Mrajishi wa vyama vya ushirika Tanzania,kuhakikisha anaunda timu ya ukaguzi ndani ya Siku 14 ili kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku katika chama cha msingi cha ushirika cha Mpanda Kati kilichopo Wilayani Mpanda.  
Waziri Nasha ametoa agizo hilo katika kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa idara ya maji Wilayani Mpanda kikishirikisha Viongoz I wa vyama vya ushirika Mpanda Kati,Kaimu mrajishi Mkoa,Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na viongozi wengine waandamizi amabo amekuja nao kutoka Wizarani.
Akizungumza mbele ya wanachama zaidi ya 100 wa chama cha ushirika Cha Mpanda Kati,Waziri Nasha ameonesha kutoridhishwa na majibu ya uongozi wa ushirika Wilaya ya Mpanda kutokana na majibu yao kutokuonesha wazi taarifa za malipo ya pesa za wakulima.
Katika malalamiko ya wakulima ni pamoja na kutolipwa pesa zao kwa awamu tofauti kutokana tumbaku yao iliyouzwa,kupunjwa kwa pembejeo za kilimo,kulipwa kwa Shilingi badala ya Dola kama wanavyoza na masuala mbalimbali kama amvyo baadhi wamebaoinisha.
Hata hivyo,kufuatia kauli ya serikali kwa mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania kumtaka kuunda timu ya uchunguzi,wakulima hao wamekuwa na maoni Tofauti kuzungumzia hatua hiyo.
Kwa nyakati tofauti wakulima wa chama hicho cha msingi wamekuwa wakilalamika kunyanayaswa kutokana na uuzaji wa tumbaku yao na malipo wanayopewa kuanzia miaka  ya 2010,ambapo kwa mjibu wa wakulima wametaka kufahamu Jumla ya shilingi milioni 600 zilipo ili walipwe pesa zao.
Hata hivyo Afisa ushirika Wilayani Mpanda Luxford Mbunda amesema kuwa hakuna pesa wanayodai wakulima wala wakulima hao hakuna deni wanalodaiwa ambapo ndicho chanzo cha sokomoko la  sintofahamu juu ya upatikanaji wa pesa hizo.
Viongozi wa Wilaya na Mkoa licha ya kuwa wanatafuta ufumbuzi wa mgogoro huo hakuna mafanikio yaliyopatikana.
Chama cha Msingi cha Ushirika cha Mpanda Kati,ni miongoni mwa vyama saba vya msingi vinavyounda chama kikuu cha Ushirika LATCU Mkoani Katavi.
Awali Waziri alipokea taarifa ya Mkoa katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi kabla ya kwenda katika ukumbi wa idara ya maji kaufanya kikao na wakulima wa tumbaku chama cha Mpanda kati.
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA MEDIA

JESHI LA POLISI KATAVI LASHAURIWA KUZUIA UHARIFU BADALA YA MATUKIO

Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, January 12, 2016

Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la polisi mkoani Katavi limeshauriwa kujenga desturi ya kuzuia uharifu kabla haujatokea badala ya kupambana na matukio
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Katavi, Dr. Ibrahim Msengi wakati wa maadhimisho ya siku ya Polisi nchini iliyofanyika Juzi katika viwanja vya Polisi Wilayani Mpanda.
Dr. Msengi amesisitiza kuwa endapo jeshi la polisi litawatumia askari wake kufanya tafiti na kushirikisha wananchi katika ukusanyaji wa taarifa, uharifu utadhibitiwa kabla haujaleta madhara.
Kwa upande wake mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi ACP Dhahiri Kidavashari amekiri kuwepo kwa mafanikio pamoja na changamoto ambazo zitafanyiwa kazi ili kuimarisha usalama.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhihiri Kidavashari aliwapongeza wananchi wanaoendelea kuonesha ushirikiano wa kuwabaini waharifu wa vitendo mbalimbali
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, January 12, 2016

Na.Issack Gerald-SUMBAWANGA
HALMASHAURI  ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imeazimia kuongeza kiwango cha ufaulu   kwa mwaka wa 2016.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na mpanda, Afisa elimu taaluma wilaya ya Nkasi  Bw. George Muhenda  amesema, kutakuwa na kikao kitakachohusisha wadau wote wa elimu ili kujadili mbinu za kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 67.79 kwa mwaka 2015 na kufikia asilimia 82 mwaka huu.
Aidha Bw. Muhenda ameongeza kuwa,walimu pia wanatakiwa kujituma bila shuruti ili kuboresha elimu.
Kwa upande wao walimu  wilayani humo ambao wameshiriki mafunzo ya namna ya kuongeza ufaulu katik masomo ya hesabu,Kiswahili na kiingereza wamesema bado kuna changamoto ya miundombinu mibovu ya elimu ikiwemo upungufu wa madarasa,madawati lakini pia ukosefu wa walimu wenye weledi wa kutosha kumudu masomo kusika.
Hata hivyo Serikali ya Wilaya ya Nkasi kwa ujumla imeiomba serikali kusaidia miundombinu mbalumbali ya madarasa na nyumba za walimu ili matokeo makubwa sasa yapatikane kwa haraka zaidi.
Wiki iliypita,zaidi ya walimu 120 walishiriki mafunzo hayo ya kuinu akiwango cha ufaulu katika shule za msingi ambapo jumla ya Halmshauri 8 za Wilaya zilihusishwa zikitokea mikoa ya Kigoma,Rukwa na Katavi.

 WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE AMPA POLE

Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, January 13, 2016

Na.Issack Gerald
WAZIRI MKUU,Kassim Majaliwa amemtembelea na kuampa pole  mke wa Baba wa Taifa,  Mama Maria Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe  Leticia Nyerere.

Akizungumza na mama Maria alipomtembelea nyumbani kwake jana(Jumanne, Januari 12,2016), Msasani jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu ametoa pole kwa  Mama Maria Nyerere pamoja na familia  na kuwaomba waendelee kuwa  wavumilivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na mpendwa wao.
“Kipindi hiki ni kigumu, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo, pia tutajumuika nanyi katika kipindi hichi chote, tuendelee kuwa watulivu na kumwomba Mungu” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Ndugu wa marehemu, John Shibuda (aliyewahi kuwa mbunge wa CHADEMA) ameeleza kutokea kwa msiba huo. Ambapo amesema “Desemba, 19 mwaka huu Leticia Nyerere alipelekwa nchini Marekani kwa matibabu na alifariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lanham, Maryland juzi saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Aidha, Shibuda amemshukuru Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kwenda kuipa pole familia na Serikali kwa namna ambavyo inatoa ushirikiano mzuri kwa familia.
Naye, Rose Nyerere amesema familia inaendelea na maaandalizi, hivyo watatoa taarifa ya baada ya kuandaa utaratibu wa siku ambayo mwili utaletwa nchini, kuagwa na hatimaye kuzikwa Butiama.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ambaye amelazwa siku kadhaa zilizopita katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa,  amesema amefarijika baada ya kumuona Waziri Mkuu huyo mstaafu akiendelea vizuri na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa kumpatia matibabu na kumhudumia vizuri.  Pamoja na kumpa pole, Waziri Mkuu amemwombea apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Naye, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kumtembelea hospitalini hapo, pia ameipongeza Serikali kwa jitihada mbalimbali inazofanya ili kusaidia wananchi na hatimaye kuiletea nchi maendeleo.
“Naipongeza Serikali kwa namna ambavyo inaendelea kutekeleza majukumu yake katika masuala mbalimbali yenye lengo la kusaidia wananchi” alisema Sumaye.
Waziri Mkuu Majaliwa, pia amemtembelea na kumjulia hali Balozi Hassan kibelloh ambaye amelazwa na anaendelea kupatiwa matibabau katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Asante kwa kuendelea kuchagua P5 TANZANIA MEDIA
Chanzo cha Habari: Ofisi ya Waziri mkuu
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, January 13, 2016

Na.Issack Gerald-Mwanza.
Jamii nchini imetakiwa kutowanyanyapaa waathirika wa dawa kulevya badala yake iwasaidie kuondokana na matumizi ya dawa hizo ikiwemo kuwafikisha katika vituo vya utimamu wa akili (Sobar House).

Rai hiyo imetolewa Bw Eddy Darkis Meneja wa Kituo cha Utimamu wa akili cha Back To Life Sobar House  Pasiansi Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, ambacho husaidia wahanga wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Bw Darkis amesema kuwa badhi ya wanajamii wamekuwa wakiwanyanyapaa wahanga wa dawa za kulevya, jambo ambalo linakwamisha mapambano dhidi ya matumizi ya dawa hizo nchini ambapo  wahanga zaidi ya 50  wamepatiwa tiba huku wengine 25 wakiendelea vizuri.
Ripoti ya Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa wa habari za kupiga vita uharifu, biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini OJADACT Bw Edwini Soko Miezi 6 ili yopita,idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya Jijini Mwanza imefikia zaidi ya watu elfu kumi.
Asante kwa kuendelea kuchagua P5 TANZANIA MEDIA
Chanzo:Mwandishi wetu Mwanza

 MAFURIKO YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA

Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, January 13, 2016

Na.Issack Gerald-MPANDA
Shule ya Msingi Nsemulwa iliyopo kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda,mpaka sasa imesajili  Jumla ya wanafunzi  513 wa darasa la kwanza na Chekechea na hatimaye kukabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa,madawati na matundu ya vyoo.

Hayo yamebainishwa na Afisa elimu kata ya Nsemulwa Bw.Gerigori John Mshota wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio shuleni hapo.
Amesema kati ya wanafunzi 513,wanafunzi wa darasa la kwanza waliopo ni 318 huku  chekechea wakiwa 195 na kufikia jumla ya wanafunzi 1945 waliopo kati shule hiyo kwa sasa  ambapo kwa uwiano wa walimu 19 waliopo,kila mwalimu anatakiwa kufundisha wanafunzi  102.
Amesema changamoto zilizopo ni upungufu wa vyumba vya madarasa 6,madawati 504 ambapo madarasa yaliyopo kwa sasa ni 7,mawati 200 huku matundu ya vyoo yakiwa 7.
Asubuhi ya leo,P5 TANZANIA MEDIA Na Mpanda Radio zimefika shuleni hapo na kushuhudia mwalimu mmoja akifundisha walimu 318 sababu kubwa ikitajwa kuwa na uhaba wa walimu.
Mwalimu Joyce Mwandega ambaye ndiye amekabidhiwa wanafunzi hao wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi Nsemulwa amezungumza na Mpanda Radio fm kutokana na hali iliyopo kuhusu wingi wa wanafunzi katika shule hiyo.
Hata hivyo ameiomba serikali na wadau wa elimu kusaidia kutatua changamoto za shule hiyo ambapo kuna uwezekano wa wanafunzi wakafikia idadi ya zaidi ya 2000 watakaokuwa katika shule hiyo tofauti na siku zote.
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, January 13, 2016

Na.Issack Gerald
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuatana na kufanya mazungumzo na mabalozi wawili kutoka nchi za Qatar na Kuwait.
 Akizungumza kwa nyakati tofauti na mabalozi hao leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amewashukuru mabalozi hao kwa pongeza walizokuja kumpatia, pamoja na namna ambavyo nchi zao zimekua zikisaidia Tanzania, ambapo ameahidi  kuendeleza ushirikiano mzuri  baina ya Tanzania na nchi zao.
Kwa upande wake, Balozi wa Qatar, Abdallah Jassim al Maadad amesema  Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo yote ambayo Qatar imepiga hatua kubwa na inaweza kutoa msaada kwa Tanzania.
Amesema Quwait iko tayari kuwekeza nchini katika sekta ya  kilimo, kwa vile ardhi ya Tanzania ni yenye rutuba na inafaa kwa shughuli za kilimo. Aidha, ametaja sekta nyingine  ambazo wangependa kuwekeza ni  pamoja na sekta ya uvuvi na viwanda.
Naye, Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem ambaye amekuja kujitambulisha kwa Waziri Mkuu, amesema nchi yake kupitia ‘Kuwait fund’ iko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Balozi  Najem, pia ameshauri vituo vya uwekezaji vya Tanzania na Kuwait kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Chanzo cha Habari:Ofisi ya Waziri Mkuu

BABA NA MAMA WA KAMBO WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA MANYANYASO NA KUMNYIMA CHAKULA MTOTO WAO

Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, January 13, 2016

Na.Issack Gerald-KATAVI
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Charles (40) Mkazi wa Kasimba anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani Katavi kwa kosa la kumnyanyasa mtoto wake anayeitwa Adam Ramadhani (17) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kashaulili sambamba na kumnyima mambo mengine ya msingi kama chakula.

 Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na  Mpanda Radio, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa Jeshi la Jeshi la polisi limeshughulikia tatizo hilo la unyanyasaji baada ya kupokea taarifa kutoka kituo cha matangazo ya Mpanda Radio FM.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa baada ya taarifa hiyo jeshi la polisi lilimpokea mtoto huyo kituoni na kuanza kulifatia suala hilo ambapo mtoto huyo alieleza kuwa alikuwa anaishi na baba yake mzazi na mama yake mlezi au wa kambo aitwaye Joyce Sino.
Kwa mjibu wa maelezo ya mtoto aliyenyanyaswa kwa nyakati tofauti alisema kuwa manyanyaso yalianza mara baada ya mama yake kufariki ambapo awali waliishi vizuri  kabla ya kifo cha mama yake lakini ghafla hali ilibadilika na akawa hapatiwi mahitaji ya kimaisha yakiwemo mavazi, chakula, matibabu na mahitaji ya shule kutoka kwa wazazi wake licha ya wazazi wake kupewa misaada kanisani na mwisho alifukuzwa na wazazi wake tarehe 29.12.2015 kwamba asikanyage kwake tena.
Baada ya tukio hilo tarehe 31.12.2015 majira ya asubuhi jeshi la polisi lilituma hati ya wito kwa baba mzazi wa mtoto ambaye baada ya kuipokea alikuja kituoni na wenzake wawili kujihami kwa kufungua taarifa ya upotevu wa tarehe 01.01.2016.
Kufuati hali hiyo,Jeshi la Polisi limefungua jalada la uchunguzi ambapo upelelezi ulikamilika na kumfikisha mtuhumiwa Ramadhani Charles mahakamani kwa kesi ya kushindwa kutoa mahitaji na uangalizi.
Kesi ya mtu huyu inatarajiwa kutajwa tarehe 01.02.2016. pia, jitihada zinafanyika za kumkamata Joyce Sino ili afikishwe mahakamani kwa kosa hilo hilo. 
Hata hivyo Kamanda wa polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari ametoa wito kwa wazazi kuacha vitendo vya unyanyasaji kabla hatua za kisheria hazijawakabidhi.
Mkoa wa Katavi,ni miongoni mwa mikoa ambayo ukatiri umekuwa ukitokea kwa nyakati tofauti.
Asante kwa kuchagu P5 TANZANIA MEDIA,Endelea kuhabarika

0 comments:

Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, January 14, 2016

Na.Boniface Mpagape-MPANDA
MKAZI wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda, Bw. Reuben Remi amefikishwa katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la kuvunja duka na kuiba nguo zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nne na elfu arobaini.

Akisoma shtaka hilo mahakamani hapo, Koplo Mtei wa jeshi la polisi Mpanda, ameiambia mahakama kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo desemba 28 mwaka jana, ambapo alivunja duka la Bi. Rosana Mwamicheta katika mtaa wa majengo mjini Mpanda.
Mbele ya hakimu David Mbembela, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama iruhusu dhamana.
Akitoa masharti ya dhamana, hakimu Mbembela amesema, mshtakiwa anatakiwa awe na wadhamini wawili ambao watawasilisha vitambulisho mahakamani, na mmoja kati yao akabidhi dhamana ya fedha taslimu shilingi laki saba na elfu ishirini na mwingine ahadi ya kiasi hicho cha fedha.
Kesi hiyo itatajwa tena January  27 mwezi huu na itaanza kusikilizwa january 28, na  Mshtakiwa amerudishwa rumande hadi masharti ya dhamana yatakapokamilika.        
Wakati huo huo,mkazi wa Kigamboni kata ya shanwe katika manispaa ya Mpanda Fredrick Josephat (18) amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la kuvunja nyumba na kuiba vitu vya ndani vyenye thamani ya shilingi laki tano na elfu sitini na saba.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 03 mwezi huu nyakati za usiku, nyumbani kwa Bw. Didas Boniface ambapo baadhi ya vitu vilikutwa kwa mshtakiwa.
Hata hivyo, mshtakiwa Fredrick Josephat amekana kutenda kosa hilo.
Hakimu David Mbembela amesema mshtakiwa ana haki ya dhamana au anaweza kujidhamini mwenyewe kwa kutoa fedha nusu ya thamani ya vitu vilivyoibwa, au mdhamini awe mtumishi wa serikali na atoe kitambulisho na ahadi ya kulipa fedha shilingi laki tano na elfu sitini na saba.
Mshtakiwa ameshindwa kutekeleza masharti hayo, na amerudishwa rumande hadi atakapokamilika masharti hayo na Kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 20 mwezi huu.
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, January 14, 2016

Na.Issack Gerald
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura. Ambapo amemuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Rwanda.

Akizungumza na Balozi  Kayihura  jana jumatano ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amemshukuru  Balozi huyo kwa kumtembelea na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano ulipo baina ya nchi hizi mbili.
“Nia yetu ni kushirikiana kwa pamoja kwa kuunganisha wafanyabiashara wetu, kwa kutumia Bandari  ya Dar es salaam na reli ya kati, ambayo tutajenga kwa  kiwango cha kisasa ‘standard gauge’  ili ziweze kubeba mizigo mingi na kwenda mwendo wa kasi” alisema Waziri Mkuu.
Kwa upande wake, Balozi wa Rwanda, Kayihura amesema Tanzania na Rwanda ni nchi marafiki na zinafanyakazi wa pamoja, Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania kikanda na kimataifa.
“Tunatumia Bandari ya Dar es salaam na Mombasa, tunashukuru kwa namna ambavyo mnaboresha Bandari ya Dar es Salaam, kwani Rwanda inafaidika pia kwa vile mizigo yetu mingi karibu asilimia 75 husafirishwa  kupitia bandari hii”  alisema Balozi Kayihura.
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, January 15, 2016

Na.Issack Gerald-MPANDA
Balaza la madiwani Manispaa ya Mpanda limetoa kauli ya pamoja kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli.

Kauli hiyo ya Madiwani,imetolewa jana katika mkutano wa balaza la pili la madiwani ambao umefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Kupitia hicho kilichokuwa kinalenga kupokea na kujadili taarifa za kamati mablimbali,baadhi ya masuala yaliyobainishwa ni pamoja na kujadili namna ya kutatua changamoto zinazoathiri wakazi wa Manispaa ya Mpanda.
Baadhi ya  changamoto hizi ni Upungufu na ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo ya Manispaa kama vile kata za Mpanda Hotel,baadhi ya maeneo ya Ilembo.
Changamoto nyingine zilizopo ni,Huduma duni za afya katika Hospitali na Zahanati,Mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi,miundombinu mibovu ya barabara zilizopo katika mipaka ya Manispaa.
Awali Mstahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Mheshimiwa Willium Philipo Mbogo  akifungua kikao hicho cha pili cha balaza hilo kwa mwaka 2016  amesema kuwa miradi mbalimbali inatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi sita iliyosalia ya mwaka  wa fedha 2015/2016.
Pamoja na mambo mengine,amesema, miradi hiyo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani,kutatua changamoto za elimu kwa shule  za Manispaa zikiwemo upungufu wa madawati pamoja na na kutekeleza mipango ya serikali.
Hata hivyo wajumbe katika balaza hilo,wameiomba manispaa kutatua changamoto za migogoro ya ardhi na kuainisha thamani ya magari mawili ya Manispaa aina ya Scania yanayotarajiwa kuuzwa mwaka huu 2016.
Wakati huo huo Suala la ukosefu wa Maji kwa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Mpanda limeonekana kuwakasirisha baadhi ya madiwani na hivyo kuhoji wajibu wa viongozi waliopewa kusimamia usambazaji wa maji safi na salama ambao ni idara ya maji MUWASA.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ambaye kisheria katika balaza la madiwani ndiye katibu,ametoa rai kwa madiwani kusambaza elimu kwa wananchi ili kuendeleza kupambana na maambukizi ya Ukimwi ambayo huenda kama takwimu zikitolewa kuna uwezekano wa kuzidi asilimia 5.9 ya maambukizi ya Ukimwi kwa sasa.
Katika hatu a nyingine Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda inatarajia kuuza magari mawili aina ya Scania huku magari mengine yatakayouzwa hayajaainishwa ni magari mangapi na aina gani.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi Manispaa ya Mpanda wamesema kuwa miundombinu ya afya,barabara,afya maji na migogoro ya ardhi inatakiwa kutatuliwa haraka.
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, January 15, 2016

Na.Issack Gerald-Mlele
Waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi Mheshimiwa Willium Tate Nashe,amewataka watumishi wa umma Wilayani Mlele Mkoani Katavi kufanya kazi kwa uadilifu,uaminifu sambamba na kuwa karibu na wananchi kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hao.

Waziri Nashe ametoa wito huo jana, alipokuwa akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali Wilayani Mlele katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele.
Aidha,Nashe baada ya kikao na watumishi wa Umma,aliendelea kuzungumza na Chama cha msingoi cha Ushirika cha Ukonongo kinachojishughulisha na kilimo cha tumbaku.
Amebainisha malengo makuu ya ziara yake aliyoianza Jumatatu ya Januari 11 mwaka huu,Mkoani Katavi kuwa ni kwa ajili ya kuja kutatua changamoto za wakulima zinazowakabili katika sekta ya kilimo,ardhi,ufugaji na uvuvi.
Wakati huo huo,ameupongeza mkoa wa Katavi kwa kuwa miongoni mwa mikoa ambayo haina historia ya njaa kwa kuwa Mkoa wa Katavi unalisha maeneo mengine yaliyokumbwa na njaa ikiwemo Shinyanga.
Waziri anaendelea na ziara ambapo leo ni siku ya tano tangu aanze ziara Mkoani Katavi ambapo ameelekea Wilayani Mlele akitokea Wilayani Mpanda baada ya kupata taarifa ya Mkoa ya  maendeleo ya  kilimo,mifungo na uvuvi na hatimaye kuzungumza na wakulima wa tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika cha Mpanda kati.
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, January 15, 2016

Na.Issack Gerald-Mpanda
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imesema kuwa mchakato wa kuhamisha Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kutoka katika utawala wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda kuwekwa katika utawala wa Manispaa unaendelea.

Hayo yamebainishwa na mganga mkuu wa Manispaa Dk.Obed Mahenge kupitia kikao cha balaza la madiwani ambacho kimefanyika jana katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Kutokana na Manispaa kutokuwa na Hospitali yake ya Manispaa,Wajumbe wa kikoa wameiomba manispaa ya Mpanda mchakato wa kuhamisha hospitali katika utawal mmoja kwenda utawala mwingine ufanyike kwa haraka ili kuwaondolea adha wananchi.
Kwa upande wake afisa anayehusika na ukusanyaji wa damu salama Manispaa ya Mpanda Bi.Redgunda Mayorwa,amesem akuwa kipindi cha  mwezi Desemba mwaka jana hadi Mwezi Januari mwaka huu,amesem akuwa kiasi ch adamu kilichokusanywa ni UNIT 407.
Katika hatua nyingine ,Dk.Mahenge amesema kuwa kata ya Kakese imeendelea kupata ongezeko la watu wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambapo kwa kipindi cha mwezi Desemba mwaka 2015 hadi Januari mwaka huu,zaidi ya watu 40 wamegundulika kuathirika.
Hata hivyo wadau mbalimbali wameshauri kuwa,kondomu,elimu ya kutosha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali viendelee kutolewa kwa wakazi wote wa Mkoa wa Katavi.
Mkoa wa Katavi una asilimia 5.9 ya maambukizi ambapo imevuka kiwango cha asilimia kwa taifa,ambapo maambukizi asilimia ya maambukizi ni salimia 5.1.
Hata hivyo kuna uwezekano wa aslimia kuongezeka ikiwa utafiti wa vipimo vya uhakika utafanyika kwa kumekuwa na ongezeko la watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Kuingia Mkoani Katavi.

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SHAMBULIO LA MME WAKE
Na.Issack Gerald-Mpanda
MTU mmoja mkazi wa Kawajense katika Manispaa ya Mpanda, Bi. Judith Mgawe, juzi amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la shambulio la kudhuru mwili dhidi ya mmewe.
Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela, Koplo Mtei wa jeshi la polisi Mpanda amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo January 8 mwaka, kwa kumpiga mmewe Bw. Kasanga Mgamba kwa kutumia kipande cha ubao na kumsababishia maumivu makali..
Hakimu Mbembela ameruhusu dhamana kwa mshtakiwa, lakini mshtakiwa alikosa mdhamini na kulazimika kudhaminiwa na Bibi yake, baada ya mahakama hiyo kulinda maslahi ya mtoto mdogo aliye naye. 
Mshtakiwa amekana shtaka hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 3 mwezi Februari mwaka huu itakaposikilizwa tena.
MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA  MWANZA AFA MAJI AKIWA NA BABAYE,ASKARI WA UOKOAJI WAKOSA MWILI
Na.Albert Kavano-Mwanza
MWANAFUNZI wa Darasa la Kwanza  katika shule ya Msingi Mabatini B Jijijni Mwanza Amefariki dunia baada ya kusombwa na maji yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha jana kwa zaidi ya saa 6,  jijini humo
Tukio hilo mlimetokea juzi majira ya saa nane mchana na kumhusisha Mtoto Janeth James Joseph (6), aliyetumbukia katika Mto mirongo baada ya kuteleza wakati akijaribu kuvuka akiwa  na baba yake.
Akizungumzia tukio hilo Mzazi wa Maerehemu Janeth, Bw James Joseph amesema kuwa ilikuwa ni siku ya pili baada ya Mwanae kuanza masomo ya Darasa la kwanza katika shule ya Msingi Mabatini B  na kukutwa na ajari hiyo wakati akitoka shule kurudi nyumbani.
Zoezi la kuutafuta mwili wa mtoto huyo kupitia vikosi vya usalama na uokaji jijini mwanza bado linaendelea na mpaka sasa Mwili huo haujapatikana .
                   Asante kwa kuchagua P5 TNZANIA MEDIA
Kwa manoni tuma kwenda geraldissack@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA