MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA MWANZA AFA MAJI AKIWA NA BABAYE,ASKARI WA UOKOAJI WAKOSA MWILI



Na.Albert Kavano-Mwanza
MWANAFUNZI wa Darasa la Kwanza  katika shule ya Msingi Mabatini B Jijijni Mwanza Amefariki dunia baada ya kusombwa na maji yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha jana kwa zaidi ya saa 6,  jijini humo.

Tukio hilo mlimetokea juzi majira ya saa nane mchana na kumhusisha Mtoto Janeth James Joseph (6), aliyetumbukia katika Mto mirongo baada ya kuteleza wakati akijaribu kuvuka akiwa  na baba yake.
Akizungumzia tukio hilo Mzazi wa Maerehemu Janeth, Bw James Joseph amesema kuwa ilikuwa ni siku ya pili baada ya Mwanae kuanza masomo ya Darasa la kwanza katika shule ya Msingi Mabatini B  na kukutwa na ajari hiyo wakati akitoka shule kurudi nyumbani.
Zoezi la kuutafuta mwili wa mtoto huyo kupitia vikosi vya usalama na uokaji jijini mwanza bado linaendelea na mpaka sasa Mwili huo haujapatikana .

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA