WAZAZI MKOANI KATAVI WATAKIWA KUWAFICHUA WATAKAOTOZA MICHANGO ILIYOPIGWA MARUFUKU SHULENI ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE



Na.Issack Gerald
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa halmashauri hiyo kuwabaini watu watakawatoza michango ya shule iliyopigwa marufuku ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Jengo la Manispaa ya Mpanda
Wito huo umetolewa na Afisa elimu Taaluma Manispaa ya Mpanda Mwalimu Rashid Pili wakati akizungumza na P5TANZANIA LIMITED Ofisini kwake kuhusu namna ambavyo wamejipanga kusimamia na kutekeleza sera ya serikali ya elimu bila malipo.
Aidha,Mwalimu Pili amesema muda wowote wanatarjia kuendesha msako wa watoto ambao hawajapekwa shule ili wazazi wachukuliwe hatua za kisheria kwa kumnyima mtoto haki ya kielimu.
Kauli ya Afisa elimu wa Manispaa ya Mpanda inakuja ikiwa ni kufuatia taarifa za hivi karibuni zilizosambaa mitaani kuwa kuna baadhi ya shule za Manispaa ya Mpanda ambazo zinakataa kumsajili mwanafunzi wa chekechea na darasa la kwanza mpaka alipe kiasi cha fedha kilichopangwa.
Manispaa ya Mpanda ina jumla ya shule 34 za serikali ambazo zinatakiwa kusimamiwa ili kuhakikisha agizo la elimu bila malipo lililotolewa na Rais Dkt.John Magufuli linatekelezeka.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA