AGIGO KALI WILAYANI TANGANYIKA



Mkuu wa wilaya ya Tanganyika  Mkoani  Katavi Salehe  Muhando ameiagiza kukamatwa kwa watu waliowazuia wananchi  160 katika kijiji cha Kaseganyama kata ya Kasekese  kufanya shughuli za kilimo katika maeneo halali.
Akizungumza na wakazi wa kijiji  hicho Muhando amesema serikali ya kijiji hicho kwa kushilikiana na serikali ya wilaya kwa pamoja waliamua kutenga hekari 1280 baada ya wananchi hao kukubali kuondoka katika maeneo ya hifadhi jambo ambalo halijafanikiwa kutokana na vitisho wa kikundi hicho.
Aidha katika  kukabiliana na uhalifu  ametoa siku kumi na nne kwa watu wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha katika ofisi za watendaji na vituo vya polisi vya wilaya hiyo kabla ya msako kuanza.
Katika ziara hiyo pia amekagua na kushiriki na wanachi katika shughuli za ujenzi wa shule ya sekondari Simbwesa na shule ya sekondari Kasekese ambazo zipo katika hatua ya renta.
Ziara hiyo ambayo aliifanya mwishoni mwa wiki iliyopita iligusia pia masuala ya kutoa elimu kuhusu sera ya elimu bila malipo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA