WANAWAKE WAANDAMANA KUPINGA UBAKAJI KATIKA HOSPITALI KENYA



Makundi ya wanawake kutoka mashirika tofuati nchini Kenya yameandamana hii leo kushinikiza serikali kuchukua hatua kuhusiana na madai kuwa akina mama waliojifungua wamekuwa wakidhulumiwa kingono katika Hospitali kuu ya Taifa Kenyatta National Hospital.
Maandamano hayo yanafanyika wakati ambapo ripoti ya uchunguzi iliyoagizwa na waziri wa afya nchini humo ikitarajiwa kutolewa rasmi.
Waziri wa afya nchini Kenya Dkt.Cleopha Mailu aliagiza uchunguzi kufanywa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada ya wanawake waliojifungua kudai kwamba wanadhalilishwa kingono.
Taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao siku ya Ijumaa zinadai kina mama waliojifungua wamekuwa wakishambuliwa na baadhi ya wafanyikazi wakati wakienda kwenye chumba cha watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao.
Wanaotuhumiwa ni wahudumu katika vyumba vya maiti, wanaonyooshewa kidole pia kwa kutumia maiti kuwashutua akina mama waliojifungua katika hospitali hiyo.
Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wanaoandamana leo katika mji mkuu, wanasema dhamira yao kuu kumiminika barabarani ni kutaka mabadiliko yafanyike, na kwamba usalama wa wanawake ni jambo linalopaswa kutiliwa umuhimu.
Mildred Atty ambaye ni miongoni mwa waandaaji wa maandamano hayo amesema tatizo hilo limekuwa likiendelea kwa muda usiojulikana na amesisitiza kuwa ni lazima liishe.
Hospitali ya taifa ya Kenyatta,Nairobi huwahudumia akina mama wajawazito 100 wanaojifungua kila siku.
Chanzo:bbc Swahili
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA