BEKI WA KAGERA SUGAR MIKONONI MWA POLISI KAGERA



Beki wa timu ya Kagera Sugar inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bra Juma Nyossoa anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kutokana na tuhuma za kumshambulia kwa ngumi shabiki hadi akazirai.
Taarifa zinaeleza,Nyosso alimshambulia shabiki huyo mara tu baada ya kumalizika kwa mechi ya jana kati ya Kagera na Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba na wageni wakashinda kwa mabao 2-0.
Wengi wanaojadili wamekuwa wakisisitiza tabia mbaya za kibabe za Nyosso zinapaswa kukomeshwa.
Lakini wengine nao wamekuwa wakihoji kama shabiki huyo alikuwa sahihi kumtukana Nyosso na inaelezwa alimsogelea hadi karibu akitoa maneno ya kashfa.
Mjadala huo unaonekana kuelemea kwa Nyosso kwa kuwa kuna mifano ya kufanya vitendo vya kihuni uwanjani.
Hata hivyo kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Josefu Olomi amesema mpaka sasa wanamshkilia mchezaji huyo kwa ajili ya mahojiano na Nyosso anatarajia kufikishwa mahakamani mara baada ya mahojiano kukamilika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA