SHUGHULI ZA KIBINADAMU MKOANI TABORA ZATAJWA KUWA CHANZO CHA UTORO SHULENI


Shughuli za kilimo,ufugaji na uelewa mdogo kwa baadhi ya wazazi wa wilaya ya SIKONGE mkoani TABORA ndiyo chanzo cha utoro wa wanafunzi na kushuka kwa kiwango cha ufaulu wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya SIKONGE,PERES MAGIRI amesema katika wilaya hiyo kuna jamii ya wafugaji ambao wanaishi mbali na huduma za kijamii zikiwemo shule, na hivyo kusababisha wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo.
Kwa upande wake,Afisa Elimu wa wilaya ya SIKONGE,HILLALY BITWALE amesema tatizo la utoro wilayani humo siyo kubwa sana na mahudhurio ya wanafunzi yanaridhisha
MAULID JUMA ni mmoja wa wanafunzi watoro sugu wilayani SIKONGE amesema hapendi kwenda shuleni kwa sababu anayofundishwa na walimu hayaelewi
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi LEMBELIkata ya KIPANGA wilayani SIKONGE,ALLY ABDI amesema wamekuwa wakiwahamasisha wanafunzi kujua umuhimu wa elimu ili kupambana na tatizo la utoro
Kufuatia wilaya ya SIKONGE kuwa ya mwisho kimkoa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana,serikali ya wilaya hiyo imesema ina mpango mkakati wa kuwaita wadau wa elimu wakiwemo walimu,wazazi na wananchi ili kupanga mikakati itakayowasaidia kuinua ufaulu wa wilaya hiyo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA