MWAKA WA FEDHA 2018/2019 MANISPAA YA MPANDA KUKUSANYA ZAIDI YA BIL.26.8



Na.Issack Gerald
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 26.8 katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo kati ya kiasi hicho mapato ya ndani yanarajia kuwa Shilingi bilioni 2.4.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mipango wa Manispaa hiyo Bi.Mary Luhulula wakati akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 kupitia kikao maalumu cha baraza la madiwani cha Manispaa ya Mpanda ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa.
Aidha Bi.Luhulula pamoja na mambo mengine amesema mwaka 2017/2018 ilikusanywa shilingi bilioni 10.4 badala ya shilingi bilioni 27.4 iliyokuwa imeidhinishwa ambapo imepanga kubuni vyanzo vya mapato ili kupata fedha ili kuchochea maendeleo.
Kwa upade wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Bw.Deodatus Kangu amesema baadhi ya tozo kurejeshwa serikali kuu ikiwemo kodi ya ardhi,mazao,mabango ya matangazo ya kijamii na baadhi ya ushuru kufutwa kumesababisha Hamlashauri ya Manispaa ya Mpanda kutofikisha asilimia 50 ya makusanyo ya mapato.
Hata hivyo Stendi Mpya ya kisasa inayotarajia kufunguliwa hivi karibuni,malipo ya papo kwa papo katika hospitali ya wilaya,Bima za afya na madawa.
Hapo kesho inatarajiwa kuchaguliwa kamati maalumu itakayosimamia ukusanyaji mapato katika Manispaa ya Mpanda ili kuchochea kasi ya kushghulikia utatuzi wa changamoto zinazokwamisha maendeleo na masuala mbalimbali ya kijamii.
Kwa mjibu wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Mbogo Kikao kinatarjia kuendelea kesho ili kujadili hoja ya matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2017.2018.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA