MOROCCO YAZINDUA KAMPENI YA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA 2026



Morocco imezindua kampeni yake ya kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya 2026 mjini Casablanca.
Morocco imezindua kampeni yake ya kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya 2026 mjini Casablanca.
Taifa hilo la Afrika kaskazini ambalo limewasilisha ombi lake la tano kuandaa fainali hizo,linakabiliwa na ushindani mkali kutoka ombi la pamoja linaloshirikisha Canada,Mexico na Marekani.
Mwenyekiti wa ombi hilo Moulay hafid Elalamy amesema Morocco itaonyesha mchezo mzuri zaidi katika kombe hilo la dunia.
Uamuzi wa atakayeandaa kombe hilo unatarajia utafanywa juni 13 mwak huu katika mkesha wa kombe la dunia la mwaka 2018 mjini Moscow.
Taifa hilo la Afrika kaskazini limefeli katika maombi yake manne miaka 1994,1998,2006 na 2010.
Mwaka wa 2010,mchuano huo uliandaliwa na Afrika Kusini huku bara hili likiandaa kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia.
Morocco inataka kubadili hayo yote na imemteua Elalamy, waziri wa serikali kuongoza ombi hilo huku aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la soka Afrika Hicham El Amrani akiwa afisa mkuu mtendaji.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA