WILAYA YA NKASI YATANGAZA VITA DHIDI YA WANAUME WANAORUBUNI WANAFUNZI KUSHIRIKI MAPENZI.

KATIKA kukabiliana na tatizo la mimba kwa wanafunzi wanaume wilayani Nkasi  Mkoani Rukwa wameonywa  kuacha mara moja tabia ya kuwaita watoto hao wa kike majina ya mahaba kwani yanawapelekea kujiona wamekua na kuanza kushiriki vitendo vya ngono.
Wito huo umetolewa jana na afisa elimu Sekondari wilayani Nkasi Abel Ntupwa  kwenye kikao kazi kilichowajumuisha Wakuu wa shule 23 za sekondari wilayani Nkasi  kilichomshirikisha na afisa elimu wa mkoa Nestory Mloka kilicholenga kupeana mikakati namna ya kuboresha taaluma baada ya wilaya Nkasi kuporomoka sana kwenye mitihani ya kitaifa.
Alisema hivi sasa watu wazima wamekua na tabia ya kuwaita watoto hao wa kike ambao ni Wanafunzi majina ya kimahaba kama  Baby kama mzaha na mwisho wa siku ujikuta Watoto hao wanajiingiza kwenye mtego huo mbaya na hivyo kuanza kushiriki vitendo vya mapenzi.
Hivyo  kufuatia hari hiyo amedai kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote  kumwita mtoto wa kike ambaye ni
Mwanafunzi majina hayo ya Baby ili kuwaweka Watoto hao katika hari ya usalama.
Lakini pia alikemea tabia ya baadhi ya Walimu wenye tabia ya kujihusisha kimapenzi na Wanafunzi au hata kuwatamani kuwa hakuna dhambi kubwa kwa Mwalimu kama hiyo na kuwa hakuna atakaebaki salama kwa kujihusisha na tabia hizo pindi itakapobainika.
Lakini pia aliwataka Wakuu wa shule kuhakikisha kuwa wao ndiyo wakaguzi wa kwanza katika shule zao kwa kuhakikisha kuwa Walimu wao wanafundisha sawasawa na kuleta tija ya kitaaluma katika masomo wanayoyafundisha.
Alisema shule yoyote inayofanya vizuri ni matokeo ya uongozi bora wa shule ambapo Walimu wakuu wameamua kuzisimamia shule zao na kuwa sasa wameamua kuboresha elimu wilayani Nkasi nas kutaka Wakuu wa shule kusiomama imara na kama kuna ambaye atakwenda kinyume na kasi hiyo  watamshughulikia mara moja.
Kwa upande wake afisa elimu wa mkoa wa Rukwa Nestory Mloka alisema kuwa yeyebinafsi kamwe hawezi kusita kuwavua madaraka Walimu wakuu ambao wataonyesha kushindwa kuzisimamia shule zao ili zitoe matokeo chanya na kuwa haoni sababu kwa wilaya Nkasi iliyokuwa inaongoza katika mkoa Rukwa sasa imeanza kushika mkia.
Alisema kwa kuanza wameanza na mabadiliko madogo ambapo wameteua baadhi ya waratibu wa elimu kata kutoka katika shule za Sekondari na msingi na kuwataka washirikiane nao vizuri na kuwa wanataka kuona mwaka huu mabadiliko yanatokea lakini kinyume cha hapo alisema kuwa hatamuelewa mtu.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA