WAMILIKI WAMABASI WAHITAJI KUKUTANA NA RAIS MAGUFULI
Wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani,wameomba kukutana na Rais John Magufuli kumweleza matatizo yanayowakabili ikiwamo vipengele wanavyodai kuwa ni kandamizi katika kanuni mpya za leseni za usafirishaji.

Akitangaza azimio hilo kwa niaba ya wajumbe waliohudhuria
mkutano huo,Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi hayo (Taboa),Enea
Mrutu,alisema wataandika barua kuomba kukutana na Rais Magufuli ili
kumweleza matatizo yanayowasibu.
Hata hivyo,Mwenyekiti wa Taboa,Mohammed Hood alisema kabla ya
kuandikia barua ya kuomba kukutana na Rais, watafanya utaratibu wa kuonana na
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa.
Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara,Johansen
Kahatano,alisema hakuna uadui kati ya Sumatra na wamiliki wa mabasi na kwamba
suala la faini inayotozwa kuanzia Sh. 250,000 hadi 500,000 na haliwezi kuingiliwa kwa sasa kwa sababu ni
la kisheria.
Aidha Kahatano aliwataka Taboa kwenda Tume ya Ushindani
kulalamika endapo wanaona kanuni au sheria hizo mpya zinawakandamiza.
Kuhusu kuzuia gari kwa kosa la dereva,Kahatano
alisema sheria ya Sumatra inasema endapo gari litakamatwa, mmiliki wa gari
atapewa siku 14 za kulipa faini hiyo na endapo siku hizo zikipita bila kulipa,mmiliki
anaweza kufika Polisi au Sumatra na kutaka kesi iende mahakamani.
Alisema hakuna gari lolote litakalozuiwa kwa kosa alilofanya
dereva na kwamba makosa ya dereva na mmiliki yametenganishwa.
Wakichangia katika mkutano huo,wajumbe wa Taboa wengi
wao walilamikia kanuni zilizokuwapo katika leseni za usafirishaji kuwa
zinawakandamiza huku wakipendekeza faini za viwango vipitiwe upya pamoja na
makosa ya dereva na mmiliki yatenganishwe
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments