WABUNGE 11 WAVULIWA UANACHAMA

Chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe jana kimetangaza kuwafukuza wabunge wake 11 ambao ni washirika wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe.

Maamuzi ya kuvuliwa uanachama wabunge hao yalitolewa na kutangazwa Bungeni na Naibu Spika wa Bunge la Zimbabwe,Mabel Chinomona baada ya Bunge hilo kupokea barau kutoka kwenye chama cha ZANU PF iliyosema wabunge hao wamefukuzwa kwa mujibu wa Katiba ya Zimbabwe kupitia kifungu namba 129 (1) (k).
Naibu Spika alisema kuwa wabunge waliofukuzwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani, aliyekuwa Waziri wa Nishati,aliyekuwa Waziri wa Michezo, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na wabunge wengine wa majimbo mbalimbali nchini humo. 
Kufuatia zoezi hilo Bunge limetangaza nafasi wazi katika majimbo hayo 11 na kuijulisha Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe kuhusu uwepo wa nafasi za wazi katika majimbo hayo kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo ili zoezi la uchaguzi liweze kufanyika kupata wawakilishi wa Wanachi. 
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA