WAFANYABIASHARA MANISPAA YA MPANDA WAANDAMANA MPAKA KITUO CHA RADIO KUMPINGA MKURUGENZI WA MANISPAA



Mmoja wa wafanyabiashara akizungumza kueleza kero(PICHA NA.Issack Gerald)
Wafanyaboiashara wakiwa wamkusanyika ndani na nje ya uzio wa studio za Mpanda Radio(PICHA NA.Issack Gerald)
Baadhi ya wafanyabiasahara wakizungumza na Mpanda Radio na kueleza kero zao(PICHA NA.Issack Gerald)
Mamia ya wafanyabiasahara wadogo wadogo  katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameandamana mpaka katika kituo cha matangazo mpanda radio wakipinga agizo la mkurugenzi wa Manispaa hiyo Michael Nzyugu  kuyafunga masoko yasiyo rasmi.

Wakizungumza na Mpanda radio mapema leo wamesema, kitendo hicho hakikubaliki kwani mpaka sasa serikali haijaandaa maeneo mbadala ya kufanyia biashara hizo.

Miongoni mwao wamesikika wakisema maeneo mengi wanayo takiwa kwenda mara baada ya kuyahama maeneo yasiyo rasimi yanakabiliwa na miundombinu dhaifu ikiwemo na mlundikano wa wajasiliamali.

Wiki iliyopita Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu  ameutangazia umma kuwa ifikapo tarehe 22 mwezi huu utakuwa mwisho wa masoko bubu maarufu kama magenge.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

 


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA