DC TANGANYIKA AONYA WATAKAOKIUKA TARATIBU ZA UCHAPAJI ALAMA ZA MIFUGO



Na.Issack Gerald
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Muhando amesema watakaokiuka zoezi la kutambua na kuweka alama ya chapa katika mifugo atashughulikiwa kwa mjibu wa sheria na taratibu za nchi.
Muhando ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaaji wa ilani ya chama cha Mpainduzi CCM katika kipindi cha mwezi Julai mpaka Desemba 2017 kupitia kikoa maalumu cha chama hicho ambacho kimefanyika Mjini Mpanda.
Aidha pamoja na mambo mengine amesema,katika kipindi cha mwezi Julai mpaka kufikia Desemba mwaka jana,zaidi ya ng’ombe 158,114 wametambuliwa na kuwekewa alama ya utambuzi katika vijiji hamsini ambapo zoezi hilo bado linaendelea katika vijiji vinne vilivyosalia Wilayani humo.
Katika hatua nyingine Muhando amesema katika kipindi cha Julai mpaka Desemba Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda imekusanya zaidi ya shilingi milioni 22,590,400 kutokana na uvuvi haramu na shilingi milioni 185,259,050 kutokana na ukamataji wa mazao ya misitu yaliyovunwa kiholela ikiwa ni pamoja na magogo,mbao na mkaa huku suala la ufugaji nyuki wilayani humo likiipatia mapato zaidi ya shilingi milioni mbili na wafugaji wenyewe wa nyuki wakinufaika kwa kupata zaidi ya shilling milioni 500.
Awali kwa upande wa wajumbe wa kikao hicho,wamesema utekelezwaji wa agizo hilo la seriikali kutambua na kupiga chapa mifugo nchi nzima litapunguza uharibifu wa mazingira,kutokomeza wizi wa mifugo na kutatua migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA