ZAIDI YA MADEREVA 300 WA PIKIPIKI WILAYANI MPANDA WAMEHITIMU MAFUNZO

Na.Issack Gerald
Madereva pikipiki maarufu kama bodaboda mjini Mpanda wameishukuru mamlaka inayosimamia usafiri wa nchi kavu na majini nchini (SUMATRA) kwa kufanikisha mafunzo ya udereva kwa madereva hao.
Mwenyekiti wa Bodaboda Mjini Mpanda Stefano Mwakabafu amesema mafunzo hayo yameendeshwa na chuo cha VETA Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya uvikama kwa hisani ya SUMATRA mkoa wa katavi.
Katika hatua nyingine amewaomba wadau wengine kujitokeza kufadhili mafunzo kama hayo katika wilaya zingine za mkoa wa Katavi ili vijana wengi waendelee kujiajiri kupitia kazi ya udereva piki piki.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamehitimshwa ambapo zaidi ya madereva 300 wamehudhuria mafunzo ambayo yamefanyikia katika shule ya msingi Azimio ilipo Manispaa ya Mpanda.

Mafunzo yalihitimishwa Desemba 5 mwaka huu yakilenga kuwapatia mafunzo ya matumizi sahihi ya pikpiki na uzingatiaji wa sheria na alama za uslama barabarani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA