MKOA WA RUKWA UMESHAULIWA KUONGEZA VITUO VYA HUDMA ZA AFYA

MKOA wa Rukwa umeshauriwa Kuongeza vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa unaoendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na ongezeko la watu.
Naibu waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Josephat Kandege alitoa ushauri huo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa huo wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi.
Alisema kuwa hivi sasa mkoa huo unaidadi kubwa ya watu hali iliyosababisha kuwepo idadi kubwa ya wagonjwa katika maeneo ya kutolea huduma za afya hivyo nilazima mkakati wakujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali uanze mara moja ilikuendana na idadi ya wakazi wa mkoa huo. 
Waziri Kandege alisema kuwa fursa nyingine iliyopo ni kuyatumia majengo yanayo achwa na makampuni ya kigeni ya ujenzi wa barabara mkoani humo kwani yakibadilishwa na kuboreshwa yanaweza kufaa kutumika kutolea huduma za afya. 
Alisema kuwa zipo baadhi ya wilaya hazina hospitali ni vizuri sasa zikajipanga kujenga ili kuwafikishia wananchi huduma karibu tofauti na hivi sasa wanazifuata mbali na kuwasababishia gharama na usumbufu mkubwa. 
Kwa upande wake Katibu tawala msaidizi wa mkoa huo Albinus Mgonya anayeshughulika na tawala za mikoa na serikali za mitaa alimwambia waziri huyo kuwa uongozi wa mkoa unamipango mingi ya maendeleo lakini changamoto kubwa iliyopo ni mapato kidogo.
Alisema kuwa halmashauri za mkoa huo zina kabiliwa na tatizo la mapato kidogo licha ya kuwa jitihada za kukusanya mapato zinafanyika ikiwemo ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato sambamba na kutumia mashine za EFDs. 

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA