DC MPANDA ATAKA JAMII KUACHANA NA MILA KANDAMIZI KWA WANAWAKE NA WATOTO

Na.Issack Gerald
Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Bi.Lilian Charles Matinga ameitaka Jamii kuachana na mila kandamizi dhidi ya wanawake na watoto wa kike.
Bi.Matinga ametoa kauli hiyo katika kilele cha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya mtoto wa kike na mwanamke. 
Baadhi ya wanawake katika kilele hicho wameelezea mimba za utotoni kuwa changamoto katika maendeleo kwa vizazi vijavyo.
Aidha wametaja nafasi ndogo ya ushiriki wa wanawake katika maamuzi ndani ya familia husababisha kuendelea kwa dhuruma dhidi ya makundi ya wanawake.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha ivungwe,kata ya katumba halamsahuri ya nsimbo yakiwa na kauli isemyo Funguka ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto haumuachi mtu salama chukua hatua.
Katika kipindi cha Mwezi Januari mpaka Juni mwaka 2017 jumla ya wanafunzi 14 wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo waliripotiwa kupata ujauzito hali ambayo ilichukuliwa kama ukatiri wa kijinsia.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA