UHABA WA WATUMISHI VITUO VYA AFYA UVINZA NA NGURUKA MKOANI KIGOMA.

VITUO vya afya Uvinza na Nguruka vilivyopo wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa watumishi katika kada zote na hivyo kuathiri ufanisi wakazi ambao unaweza kusababisha vifo kwa wagonjwa wanaohitaji huduma katika vituo hivyo.
Zena Shaban na Mapinduzi Hamisi ni baadhi ya wananchi katika wilaya ya uvinza ambapo wameiamba mpanda redio kero wanazo kumbana nazo namapendekezo yao kwa serikali.
Stanford Chamgeni ambaye ni mganga mfawidhi wa kituo cha afya Nguruka amesema wanakumbana na kazi kubwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa ambapo kwa siku hutoa huduma kwa wagonjwa 80 hadi 100 huku mganga wa Kituo cha afya Uvinza Albert Msingwa akielezea upungufu wa majengo katika kituo chake.
Naye Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Albert Mumwi amekiri mapungufu hayo na kuelezea kuwa kufikikia sasa tayari wauguzi 10 wamepatiwa ajila na tayari wamepangiwa vituo vya kazi.
Tatizo hilo la upungufu wa watumishi limetajwa kuwa kero ya muda mrefu katika vituo vya afya wilayani uvinza huku idadi ya wakazi ikikadiriwa kuwa 178,189 huku waganga katika wilaya hiyo wakiwa saba na vituo vya kutolea huduma vikiwa 5.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA