WILAYA YA MPANDA IMETENGA HEKA ZAIDI YA 7000 KWA AJILI YA WALIOONDOLEWA KATIKA MAENEO YA HIFADHI

Na.Issack Gerald
Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Lilian Matinga amesema zaidi ya heka elfu saba zimetengwa kwa ajili ya wananchi walioondolewa katika maeneo ya hifadhi za misitu. 
Bi.Matinga amesema kitendo cha uvamizi wa misitu ni uhalifu na kwamba kila mwananchi anapaswa kuishi mahali popote kwa kufuata sheria.
Katika hatua nyingine amewaonya baadhi ya viongozi wanao warubuni wananchi ili kuyarudia maeneo hayo kuacha maramoja na kuwatadharisha kuwa sheria itachukua mkondo wake.
Awali baadhi ya viongozi wa kata ya Stalike ambayo vitongoji vyake vimekumbwa na sakata hilo wamekana kuwepo kwa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya wananchi hao ambao wanaishi porini.
Sanjari na hayo viongozi hao wameshutumiwa na wananchi kwa kitendo cha kuwachangisha fedha kwa madai ya kutaka kuonana na waziri Mkuu ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA