VIKUNDI ZAIDI YA 40 VYA WAJASILIAMALI WAJANE MKOANI KATAVI VIMEZINDULIWA,MBUNGE AVIPATIA MTAJI WA KIANZIO

Na.Issack Gerald
Mbunge wa viti maalumu mkoani Katavi Taska Mbogo(CCM) amewataka wanawake kujiunga katika vikundi mbalimbali ili wapatiwe mikopo itakayowasaidia kumudu hali ngumu ya kimaisha.
Mbogo ametoa wito huo wakati akizindua vikundi cha wajasiriamali vya wakina mama wajane zaidi ya 40 kutoka mitaa ya msasani,tambuka reli na mpanda hoteli.
Katika uzinduzi huo amegawa mtaji wa gunia tatu za mchele na pesa zaidi ya shilingi laki moja kwa ajili ya kusajili vikundi vyao.
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM(UWT) kata ya mpanda hoteli Bi.Elika George ambaye ni miongoni mwa wanakikundi hao amesema kujiunga katika vikundi hivyo kutawasaidia kujikwamua kimaisha na kuondokana na hali ya kuwa omba omba.
Bi.George amewashauri akina mama wenzake kujikita zaidi katika malengo ya shghuli zitakazowakwamuakiuchumi.
Kwa upande wao akina mama mbali na kumshukuru mbunge kwa mchango wake wamesema watadhititi vema kutumia mtaji huo katika kujiendeleza ili waondokane na umaskini.
Kuundwa kwa vikundi hivyo ni baada ya kauli ya halmasahuri ya Manispaa ya Mpanda kuwataka wakazi wa Manispaa hiyo kuunda vikundi vya kijasiliamali ili wapatiwe mikopo ambapo katika asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri,asilimia 5 inatolewa upande wa wanawake na 5 nyingine upande wa vijana.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA