WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI IMEWATAKA WAVUVI WAKACHUKUE INJINI BOTI WAVUE SAMAKI KWA TIJA

Na.Issack Gerald
SERIKALI imetoa wito kwa wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania waliopo mwambao wa bahari na maziwa kuhamasisha vikundi vya wavuvi waliopo katika maeneo yao kupitia Halmashauri zao kujitokeza na kuchukua ruzuku ya boti injini 24 zilizobaki kwa ajili ya kuendesha shughuli za uvuvi zenye tija.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na naibu waziri wa mifugo na uvuvi Mh.Abdallah Hamis Ulega wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Vijijini Mh.Moshi Suleiman Kakoso aliyetakakujua  ni lini serkal;I itawapatia vitendea kazi wavuvi wadogowadogo.
Pamoja na mambo mengine Mh. Abdallah Hamis Ulega akijibu swali hilo amesema kwa mwaka wa fedha Mwaka wa fedha 2015/2016 serikali ya awamu ya tano ilitenga shilingi 400 zilizonunua boti injini 73 ambapo kati ya hizo injini 49 zilishachujkuliwa na vikundi vya uvuvi  nchini kwa mtindo wa ruzuku kupitia Halmashauri zao ambapo serikali inachangia 40 na vikundi 60%.
Naye Mbunge viti maalumu Mkoani Katavi Anna Lupembe amemwomba  wizara kufika katika maeneo ya  Ikola,Karema,Kapalamsenga na maeneo mengine yanayoendesha shghuli za uvuvi ili kusikiliza keromzao suala ambalo waziri  Abdallah Hamis Ulega amemjibu kuwa baada ya kikao cha tisa wafika ziwani Tanganyika ili kusikiliza kero ili zitatuliwe.
Kwa upande wake Zainabu Katimba Mbunge viti maalumu Mkoani Kigoma  baada ya kuuliza swali akitaka kutambua  hatua zinazofanywa na serikali kuhakkikisha wavuvi wanazifikia fursa mbalimbali,waziri Abdallah Hamis Ulega amesema kwa mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imekwishatenga shilingi milioni 100 ili kuendelea kusaidia vikundi vya uvuvi vitakavyokuwa vimeundwa.  

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA