SHIRIKA LA WORLD VISION KUKABIDHI VIFAA TIBA KWA VITUO VYA AFYA 111 MKOANI

Na.Isaac Isaac-Kigoma
Jumla ya vituo vya afya 111 vintarajiwa kunufaika kwa kupatiwa vifaa tiba pamoja na ujenzi wa wodi na vyumba vya upasuaji katika wilaya tatu (3) za mkoa wa Kigoma.
Kigoma Ujiji
Hatua hiyo ni kupitia mradi wa uboreshaji wa huduma ya mama na mtoto unaofadhiliwa na shirika la World Vision lengo likiwa ni kutoa hamasa kwa wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya.
Kauli hiyo imetolewa na meneja mradi Monica Dedu kutoka katika shirika la world Vision wakati wa semina elekezi kwa viongozi wa madhehebu ya kidini pamoja na madiwani  katika Manispaa ya Kigoma ujiji ili kutia moyo na kuhamasisha  jamii kuona umuhimu wa kutumia huduma za afya.
Naye Mganga mkuu wa mkoa Kigoma Poul Chaote amesema asilimia 65 ya akina mama wajawazito ndio wanaofika katika vituo vya afya kwa ajili ya kujifungua huku wengine wakijifungulia majumbani jambo linalohatarisha afya zao lakini pia usalam wa maisha ya watoto
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa kidini wamesema serikali bado ina jukumu la kuweka miundo mbinu bora katika maeneo  ya vijijini kwa kuwa ndio sehemu ambazo kuna kiwango kikubwa cha vifo vya akina mama na watoto ambapo wamesema jambo hilo litasaidia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto mkoani kigoma.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA