MIMBA KWA WANAFUNZI KAA LA MOTO KWA WAZAZI NA WANAFUNZI MKOANI RUKWA

Na.Issack Gerald
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa shule mkoani humo kumkamata na kuwaweka ndani Mzazi na Mwanafunzi yeyote wa kike atakayebainika kuwa na mimba hadi hapo watakapomtaja anaehusika na mimba hiyo.
Amesema kumekuwa na tabia ya kumalizana kienyeji huko majumbani na matokeo yake Watuhumiwa hawafikishwi sehemu husika ili waweze kuwajibishwa.
Ametoa agizo hilo baada ya kusomewa taarifa ya Shule ya sekondari Kilando iliyopo Wilayani Nkasi wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa maabara pamoja na kuongea na Wanafunzi, na kupewa taarifa ya mimba saba kwa kipindi cha January hadi October mwaka huu wa 2017 huku kesi zote zikiwa zimefikishwa polisi.
Alitahadharisha kuwa shule yoyote atakayoitembelea katika ziara yake hiyo ya kujitambulisha katika Halmashauri nne za mkoa huo,ihakikishe inabainisha hatua zilizochukuliwa kwa Watuhumiwa na zilipofikia na si kueleza tu idadi ya kesi na kuwepo kwa kesi hizo polisi.
Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilando Erneo Mgina amesema kati ya Wanafunzi saba waliopata ujauzito Wanafunzi watatu ni wa “A – Level” na wanne ni wa “O – Level” na kueleza kuwa wengi wao hupata mimba wakati wa likizo na huwabaini pale tu wanaporudi shule na kuwapima.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA