BAADA YA HUKUMU YA LULU,MAMA WA MAREHEMU KANUMBA AZUNGUMZA

Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema leo atakwenda makaburi ya kinondoni alipoziikwa mwanaye ili kumzika upya.
Mama wa Marehemu Kanumba
Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo.
"Kwa sasa sina la kusema ila  naishukuru sana Mahakama kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba". Mama Kanumba
Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.
Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA