SERIKALI YATOA TAHADHARI UGONJWA HATARI WA DENGUE


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amewashauri wananchi kwenda vituo vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue.
Mhe.Ummy Mwalimu
Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki,Kati na Kusini ECSA leo jijini Dar es salaam.
“Kuna dalili za Ugonjwa Dengue zikiwemo homa ya ghafla,kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu.Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo.Wizara inashauri wananchi wasiwe na hofu,bali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa waende katika vituo vya tiba"amesema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema wakati mwingine dalili za ugonjwa huo zinaweza kufanana sana na dalili za malaria hivyo wananchi wanaaswa kwamba,wakipata homa wahakikishe wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria au Dengue,au sababu nyingine,ili hatua stahiki zichukuliwe.
Waziri Ummy amesema ili kujikinga na ugonjwa huo ni lazima Kuangamiza mazalio ya mbu kwa kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo pamoja na Kujikinga na kuumwa na mbu kwa  kuvaa nguo ndefu muda wote hasa nyakati za mchana.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA