RAIS AWAAPISHA MABALOZI WAWILI AKIWEMO IGP MSTAAFU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amewaapisha Meja Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi na IGP Mstaafu Ernest Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda.
Hafla ya kuwaapisha Mabalozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza baada ya kuapishwa Mhe.Balozi Mumwi amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa uteuzi huo na ameahidi kuwa katika kipindi chake atahakikisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi unaimarishwa na Tanzania inanufaika na uhusiano huo ikiwemo kuvutia uwekezaji katika viwanda.
Kwa upande wake Mhe.Balozi Mangu pamoja na kumshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kumuamini ameahidi kuongeza msukumo katika utekelezaji wa ajenda muhimu za maendeleo kati ya Tanzania na Rwanda hususani ujenzi na manufaa ya mradi mkubwa wa reli ya kati utakaoiunganisha bandari ya Dar es Salaam na nchi nne za magharibi mwa Tanzania ikiwemo Rwanda. 
Kwa upande Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Dkt.Susan Kolimba amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuiwakilisha Tanzania nchini Urusi na Rwanda na ameahidi kuwa wizara hiyo itakuwa tayari wakati wote kutoa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo diplomasia ya uchumi.
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan amewataka Mabalozi hao kufuatilia na kusimamia kwa ukaribu makubaliano mbalimbali ambayo Tanzania na nchi hizo wameyafikia ikiwemo miradi ya maendeleo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA