RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MMILIKI WA TIGO,VIGOGO WA UJERMANI NA DENMARK NAO WAJITOKEZA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli amekutana na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom International Services LLC inayomiliki kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Bw.Mauricio Ramos,Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kwa mjibu wa taarifa ya mawasiliano ya ais Ikulu wamezungumza kuhusu uwekezaji wa kampuni hiyo hapa nchini.
Kwa upande wake Bw.Mauricio Ramos amesema amekuja kumweleza Mhe.Rais Magufuli kuhusu maendeleo ya kampuni hiyo ambayo imewekeza Dola za Marekani zaidi ya Bilioni 1 (sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 2.23 za Tanzania) katika miaka mitano iliyopita na imeajiri wafanyakazi zaidi ya 90,000 na kuwafikishia mawasiliano Watanzania kwa takribani asilimia 90.
Aidha Bw.Mauricio Ramos amempongeza Mhe.Rais Magufuli kwa jitihada zake za kupambana na rushwa na amebainisha kuwa juhudi hizo ni muhimu katika kuharakisha maendeleo na kupunguza umasikini.
Naye Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa amesema kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ni ya pili kwa ukubwa hapa nchini ikiwa na wateja Milioni 11.06 na imekuwa ikilipa vizuri kodi ambapo mwaka 2017 ililipa kiasi cha Shilingi Bilioni 262.77.
Katika hatua nyingine,Mhe.Rais Magufuli amekutana na watendaji wakuu wa kampuni ya Ferrostaal kutoka nchini Ujerumani na Denmark na Watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Nishati, ambapo wamejadili kuhusu mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea Mkoani Lindi.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage,Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Medard Kalemani na Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe.Einar Hebogard Jensen.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA