NECTA YABADILI MFUMO MTIHANI DARASA LA SABA


Baraza la Mitihani Tanzania Nacte,limefanya mabadiliko katika mfumo wa kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi .
kwa wanafunzi wa darasa la saba nchini.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Dk Charles Msonde.
Mabadiliko hayo yamefanywa jana na Baraza hilo na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Dk Charles Msonde.
Ofisa Habari wa Necta,John Nchimbi amesema mabadiliko hayo yametangazwa na Dk.Msonde katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika Dodoma.
Nchimbi amesema katika muundo huo mpya kila somo litakuwa na maswali 45 ambapo kati ya hayo,maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na matano yatakuwa ya kujieleza/kuonyesha njia na jibu.
Amesema katika maswali 40,kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yakijibiwa kwenye OMR FORM huku maswali matano yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.
Kutokana na muundo huo mpya,Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA