MEI MOSI KITAIFA KUFANYIKA JIJINI ARUSHA


Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda,Biashara,Taasisi za Fedha,Huduma na Ushauri (Tuico),kimeanza maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) mwaka 2018.

Akizungumza katika semina ya kuelimisha na kubadilishana uzoefu iliyowashirikisha viongozi wa matawi mbalimbali ya  Tuico mwishoni mwa wiki,jijini Dar es salaam,Mwenyekiti wa Tuico taifa,Sangeze alisema Shirikisho la Vyama vya Huru vya Wafanyakazi nchini (Tucta),limekiteua chama chao kuwa mratibu wa shughuli zote za Mei mosi kwa mwaka huu.
Alisema baada ya kupewa fursa hiyo wanafanya vikao vya maandalizi na tayari wamepanga maadhimisho hayo kwa mwaka huu.
Katibu wa Tuico Boniface Nkakatisi,alisema maandalizi hayo yanaenda na mialiko ya wageni watakaohudhuria ikiwamo wafanyakazi mbalimbali nchini,wanachama  wa Tuico,mabalozi kutoka nchi mbalimbali duniani.
Mwenyekiti wa Tuico taifa,Paulo Sangeze alisema mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli ambapo kitaifa yatafanyika mkoani Arusha katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA