TMA YATOA ANGALIZO



Mamlaka ya hali ya hewa nchini imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa mvua kubwa katika baadhi ya mikoa ya Rukwa, Mbeya,Songwe,Iringa,Njombe na Ruvuma kuanzia leo usiku.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa.
Aidha taarifa hiyo inaonesha mawimbi makubwa yanayozidi mita 2 vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga, Dar es Salaam,Pwani,Lindi,Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mamlaka ya hali ya hewa ipo chini ya Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano hapa nchini.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA