KENYA YAZUNGUMZIA UAMUZI WA KUMFUKUZA MIGUNA



Wizara ya mambo ya ndani nchini Kenya imesema wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna alipata hati ya kusafiria ya Kenya kinyume cha sheria na hivyo kutimuliwa kwake kwenda nchini Canada hakukukiuka sheria za nchi wala haki zake.

Jana usiku mamlaka nchini Kenya zilimfukuza ghafla Miguna na kumpandisha katika ndege ya shirika la Uholanzi la KLM kuelekea nchini Canada. Hatua hiyo ilizua mjadala mkubwa huku wengi wakiilaani serikali ya Kenya kuwa ilikiuka sheria za uhamiaji za nchi hiyo na haki za kiraia za bwana Miguna
Katika taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Kenya msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka amesema bwana Miguna "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wan chi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009.
Miguna alifukuzwa nchini Kenya mara baada ya kushiriki katika kiapo kisicho rasmi cha Raila Odinga kuwa rais wa watu wa Kenya mwezi uliopita.
Odinga ni mwanasiasa wa upinzani ambaye alisusia marudio ya uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika mwaka jana, kwa madai kuwa haukuwa huru na wa haki.
Rais Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi kwa kura nyingi katika uchaguzi huo

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA