JAJI MKUU WA KENYA AILAUMU SERIKALI YAKE KUKIUKA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI


Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha sheria na katiba ya kenya katika kukabiliana na upinzani.
Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga
Tamko hilo limekuja mara tu baada ya kiongozi mmoja wa upinzani wakili Miguna Miguna kufukuziwa nchini Canada,baada ya kuzuiliwa na polisi kwa siku tano hata baada ya mahakama kutoa amri kwamba aachiliwe kwa dhamana .
Katika maelezo yake jaji David Maraga,amesema malalamiko yaliyopelewekwa mahakamani yalikuwa wazi,na yalikuwa majukumu ya mahakama kufanya maamuzi kwa kuwa ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe.
Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama.
Kwa mjibu wa madai ya serikali ya Kenya ni Kwamba Miguna Miguna alishakana uraia wa Kenya na kuchukua uraia wa Canada ambapo kata hivyo kwa mjibu wa katiba ya Kenya raia wan chi hiyo anaruhusiwa kuwa na u8raia wan chi mbili.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA