BEI MPYA YA MAFUTA INAYOANZA KOTE KUTUMIKA NCHINI




Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo Februari 7 huku bei za petroli,dizeli na mafuta ya taa zikipanda.
Taarifa ambayo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura Nzinyangwa Mchany amesema bei za rejareja zimeongezeka kwa petroli ikiwa ni Sh59 sawa na 2.70%,dizeli Sh46 sawa na 2.30%,na mafuta ya taa kwa Sh24 sawa na 1.17%.
Wakati huo huo amesema bei za jumla nazo zimeongezeka ambao kwa petroli ni Shilingi 58.57 sawa na 2.85%,dizeli kwa Shilingi 46.48 sawa na 2.44% na mafuta ya taa kwa Shilingi 23.75 sawa na 1.24%.
Mchany amesema ongezeko hilo linatokana na bei kuongezeka katika soko la dunia.
Amesema bei za rejareja katika mikoa ya Kaskazini zimeongezeka,ambapo petroli ni kwa Shilingi15 sawa na 0.70% na dizeli kwa Shilingi 47 sawa na 2.29%.
Kwa upande wa Bei za jumla zimeongezeka petroli ikiwa ni kwa Shilingi 15.36 sawa na 0.73% na dizeli Shilingi 47.18 sawa na 2.42%.
Katika hatua nyingine Mchany amesema sehemu ya shehena kubwa ya mafuta yaliyopokelewa katika Bandari ya Dar es Salaam ni yenye bei ya soko la dunia za Novemba,2017 wakati iliyopokewa katika Bandari ya Tanga ni ya bei ya soko la dunia ya Desemba 2017.
Amebainisha kuwa bei za mafuta katika soko la dunia kwa Novemba 2017 ziko juu kwa zaidi ya asilimia 6 ikilinganishwa na bei za Oktoba 2017 wakati bei za Desemba zina mabadiliko tofauti.
Amesema bei ya petroli imepungua kwa asilimia 0.2 na ya dizeli na mafuta ya taa imeongezeka kwa asilimia 2.7 na asilimia 1.9.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA