KIONGOZI NRM KENYA APANDISHWA NDEGE KWA LAZIMA KUTOKA KENYA MPAKA KANADA AKIHUSISHWA NA KIAPO CHA RAILA


Mwanasiasa wa muungano wa upinzani nchin Kenya Nasa, Miguna Miguna amefukuzwa na kupelekwa nchini Canada kupitia ndege ya KLM.
Serikali yamfurusha Miguna Miguna na kumpeleka Canada
Kwa mjibu wa mawakili wa Miguna Nelson Havi na Cliff Ombeta Ombeta waliarifiwa kuwa Bw.Miguna aliingizwa katika ndege iliokuwa ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada huku wakili mwingine Dkt.John Khaminwa akisema mteja wake tayari ameondoka Kenya.
Haijulikani ni sheria gani iliyotumiwa na serikali kumuondoa nchini Kenya kwa kuwa katiba inampatia haki kama raia wa Kenya kwa kuwa ni mzaliwa wa taifa hilo.
Kwa mjibu wa mawaikili hao,wakati Miguna alipokamatwa serikali ya Canada ilikuwa imeiandikia Kenya kionyesha wasiwasi kwamba raia wake alikuwa ananyanyaswa na walitaka arudishwe nchini humo.
Siku ya jana Bw.Miguna alisema alikamatwa bila mawasiliano na familia yake ama wakili wake kwa siku tano akisema kuwa kuwa maafisa wa polisi walimnyanyasa kwa kumfungia katika maeneo ambayo hayafai kwa binaadamu.
Ripoti za kufurushwa nchini Kenya zilijiri saa chache baada ya jaji wa mahakama kuu Luka Kimaru kumzuia mkurugenzi wa Ujasusi na inspekta jenerali wa polisi dhidi ya kumwekea mashtaka yoyote.
Jaji huyo awali alikuwa ameamuru kwamba inspekta jenerali wa polisi na mkurugenzi wa shirika la ujasusi walikuwa wamekiuka agizo la mahakama lililowataka kumwachilia kiongozi huyo.
Huku Jaji huyo wa Kajiado akiagiza awasilishwe mbele ya jaji Kimaru katika mahakama ya Milimani,bwana Miguna hakuwasilishwa katika mahakama hiyo huku mawakili wake wakilazimika kusubiri hadi usiku wakisubiri kuachiliwa kwake.
Miguna alikamatwa Ijumaa iliopita huku jaji wa mahakama kuu James Wakiaga akimwachilia kwa dhamana ya ksh. 50,000 lakini hakuachiliwa.
Mkurugenzi wa shirika la ujasusi baadaye alisema kuwa bwana Miguna alikamatwa baada ya kukiri kumpatia kiapo kiongozi wa Nasa Raila Odinga mbali na kuwa mwanachama wa kundi lililopigwa marufuku la NRM.
Mgiuna alikamatwa siku ya Ijumaa kwa tuhuma za kushiriki katika sherehe ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye aliapishwa kuwa rais wa wawananchi Januari 30 mwaka huu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA