ZIMAMOTO NA UOKOAJI-TAFUTENI VIBALI KABL YA KUJENGA


Na.Issack Gerald-Katavi

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Katavi limetoa wito kwa wananchi  kupata vibali vya ujenzi wa nyumba zao ili kupunguza ujenzi holela.

Hayo yamebainishwa na kamishina msaidizi jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa katavi Kuhindi ambapo amesema majanga mengi yanatokea kwa kutofuata taratibu za namna bora ya ujenzi wa makazi.

Amesema wananchi wanaojenga bila kufuata taratibu na kupata kibali wanasababisha ugumu wa uokoaji katika maeneo hayo pindi majanga mbalimbali yanapotokea.

Hata hivyo amesema kupungua kwa gharama kutoka kiasi cha shilingi 150,000 hadi Shilingi 50,000 kumetokana na tathimini ya muda mrefu ambayo ililenga kuondoa vikwazo kwa kundi kubwa la wananchi ambao wasingeweza kumuda gharama hizo.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA