AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUBAKA MWANAFUNZI


Na.Issack Gerald-Katavi
Mahakama ya wilaya ya  Mpanda  Mkoani Katavi  imemuhukumu kifungo cha maisha Lazaro Ngomalala(50)mkazi wa  Kijiji cha Sibwesa  wilayani Tanganyika baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili(9)wa shule ya msingi Sibwesa.
Akisoma hukumu hiyo juzi,hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Chiganga Tengwa alisema mahakama imeridhika na ushahidi wa  mashahidi  sita wa upande wa mashitaka  uliotolewa mahakamani hapo ukiwemo wa mwanafunzi aliyebakwa.
Kabla ya kutoa hukumu  hiyo Hakimu  Tengwa  alisema mtu  yoyote  anayefanya kitendo kama alichofanyiwa  mtoto huyo  anakuwa  amefanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha sheria   namba 130(1)na(2) na kifungu cha  sheria namba 131(3) cha  kanuni ya adhabu.
Hakimu Tengwa  alisema  miongoni mwa ushahidi uliosababisha mahakama imtie hatiani mtuhumiwa ni  ushahidi  uliotolewa na mtoto aliyebakwa pamoja  na mtoto mwenzake mwenye umri wa miaka saba  licha ya kuwa na umri mdogo  walitoa ushahidi  kwa ufasaha  mkubwa dhidi ya tukio hilo.
Pia  Mahakama  ilijiridhisha na  ushahidi uliotolewa  na   muuguzi wa   Zahanati ya Sibwesa  aliyeamchunguza na kubaini kuwa kubaini mtoto  huyo  alikuwa  amembakwa  alimwanzishia dawa ya kuzuia  maambukizi ya virus vya ukimwi.
Katika kujitetea mtuhumiwa ,aliiomba  Mahakama  kumwachia huru akidai yeye  hakutenda kos  hilo  bali   alisingiziwa na  mama  mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa  alikuwa akimdai fedha  alizomkopesha.
Baada ya  utetezi huo hakimu Tengwa  alisema kutokana   na mshitakiwa  kupatika  na  hatia Chini ya kifungu  cha   sheria namba131(3),mtu yoyote  atakae  mbaka  mtoto mwenye umri wa miaka chini ya (10)  adhabu yake ni kifungo cha maisha  jela.
Hivyo kutokana  na  mshitakiwa Ngomalala kupatikana  na  kosa  hilo  mahakama imemuhukumu kuanzia  jana  kutumkia kifungo cha  maisha jela.
Awali  kwenye  kesi  hiyo  Wakili wa  Serikali  Fravian  Shiyo  alidai   Mahakamani  hapo kuwa   Lazaro alitenda kosa  hilo Oktoba  12  mwaka  jana  majira ya saa 4 asubuhi kijijini hapo.
Ilidaiwa kuwa  siku ya  tukio  mshitakiwa  alikuta  mtoto aliyemtendea  kitendo  hicho  akiwa na mtoto  mwenzake wakiwa wanacheza  jirani na  nyumba yao ndipo  alipowadanganya wafuate  nyumbani kwake  ili akawape fedha wakanunue biscuit na  soda.
Mwanasheria  aliiambia  mahakama  hiyo baada ya kufanyiwa  kitendo  hicho mtoto  huyo  aliyebakwa alikwenda kutoa  taarifa kwa wazazi wake  huku akiwa  analia na wazazi wake walitoa  taarifa kwa askari  mgambo wa  kijiji ambaye alimkamata na kumfikisha kituo cha  polisi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA