WAZIRI WA ELIMU AMETOA AGIZO KALI KWA WAKUU WA VYUO ELIMU YA JUU



Na.Issack Gerald
Serikali imewaagiza wakuu wote wa vyuo vya elimu ya juu kuacha urasimu katika utoaji wa fedha kwa wanufaika wa mikopo ambao wana makubaliano na Serikali.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema leo bungeni ikiwa ni utekelezaji  wa agizo la Spika Job Ndugai  lililotaka serikali kutoa kauli kuhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutakiwa kutoa fedha ili wasajiliwe kabla ya kupata  mikopo.

Agizo la Spika lilitokana na Mwongozo uliombwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata ambaye alieleza bunge kuwa wanafunzi wamekuwa wakihangaika vyuoni baada ya kutakiwa walipe fedha za usajili kabla ya kupewa mkopo.
Amesema inasikitisha sana kuona baadhi ya vyuo vinadiriki hata kuwakataa wanafunzi waliowadahili wao wenyewe au vinawalazimisha wachukue programu tofauti na walizokuwa wamechaguliwa awali na vyuo husika.
Amesema Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa vyuo vyote vitakavyoleta usumbufu usio wa lazima kwa wanafunzi na kuwafanya wapoteze muda ambao wanapaswa kuutumia kwa masomo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA