WAKAZI MKOANI KATAVI WAMETAKIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA UMEME



Na.Issack Gerald-Katavi
Wakazi wa mkoa wa Katavi wametakiwa kuwa walinzi wa kutunza miundo mbinu ya umeme ili wapate huduma nzuri na kupunguza kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Wito huo umetolewa na meneja wa shirika la umeme (TANESCO) mkoani katavi mhandisi Julius Sabu ambapo amesema wananchi wamekuwa wakichangia kuharibika kwa miundombinu hiyo.
Ametaja baadhi ya magari marefu kuwa miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha kukatika nyaya za umeme na hivyo kusababisha hitilafu na hatimaye usumbufu kwa watumiaji wa nishati hiyo muhimu.
Aidha amesema shirika la umeme linafanya utaratibu wa kutenganisha laini za makazi ya watu na maeneo ya viwandani ili kuondosha tatizo la kukatika kwa umeme unaotokana na matatizo yanayosababishwa na viwanda kutumia laini moja na watumiaji wa kawaida.
Hata hivyo amewaomba wananchi kujenga tabia ya kutoa taarifa pale wanapoona kuna shida ya umeme katika maeneo yao ili kurahisisha kazi na kutatua changamoto kwa haraka.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA