WANAFUNZI SHULE YA BIBLIA FPCT KATUMBA WAMETEMBELEA KITUO CHA MPANDA RADIO,MENEJA WA KITUO ATOA NENO KWAO

Na.Issack Gerald

Wanafunzi 17 walimu 3 wa shule ya biblia FPCT Katumba Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wametembelea kituo cha Mpanda Radio na kueleza kuridhishwa na namna  kinavyosaidia jamii katika masuala mbalimbali ya kijamii.

Kutoka Kushoto WA PILI aliyevaa kitambulisho ni Issack Geral,anayefuata aliyeweka mkono mfukoni ni Meneja wa Mpanda Radio Levocatus Msafiri,mwenye shati ya mikono mifupi aliyeshika kifuani ni mkuu wa vipindi Mpanda Radio Edward Mganga na waliobaki ni wanafunzi isipokuwa aliye karibu na Edward kutoka kulia ni Mkuu wa Shule Mch.Elisa Musenda(PICHA NA.Issack Gerald)

Mara baada ya kutembelea kituo hiki,Mkuu wa shule ya biblia FPCT Mchungaji Elisha Musenda pamoja na kuipongeza  Mpanda Radio kwa namna inavyohudumia wananchi amesema kuna kila sababu ya kituo hicho kufika mbali zaidi kimatangazo.

Kwa upande wake Meneja wa kituo cha Mpanda Radio Bw.Levokatus Msafiri,amesema kituo kitaendelea kushirikiana na kila mwananchi kwa lengo la kuchochea maendeleo bila kujali itikadi ya mtu.

Aidha  Meneja Msafiri ametoa wito kwa wanafunzi hao ambao pia ni viongozi wa dini katika maeneo wanayotka kutumia nafasi yao waliyonayo kuelimisha jamii namna ya kuondokana na tatizo la mimba za utoto,Kutumia vyandarua kujikinga na mbua waenezao maralia  pamoja na mapambano dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa hatari wa Ukimwi kutokana na Mkoa wa Katavi kuwa mkoa wenye hali ya kiwango cha juu katika matatizo hayo.
Kwa upande wake Kalenga Jailos ambaye mwenyekiti wa wanafunzi waliofika katika kituo cha Mpanda Radio akizungumza na kwa niaba ya wanafunzi wenzake amewashauri watnazania kutumia Mpnda Radio kwa kuwa ipo kwa ajili ya kuwahudumia .

Mpaka sasa Mpanda Radio imetimiza miaka minne tangu ianze kurusha matangazo yake mwaka 2013.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA