JELA MIAKA 30 MKOANI RUKWA KWA KOSA LA KUBAKA MTOTO

MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30  Jela,kulwa Dase (35) mkazi wa kijiji cha Paramawe wilayani Nkasi kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 15.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama hiyo Ramadhan Rugemalila alisema mahakama imeridhishwa pasipo kuacha shaka yoyote na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hivyo kumuhukumu mtuhumiwa kifungo hicho.
Alisema kufuatana na mwenendo wa kesi hiyo ambapo mashahidi wanne walitoa ushahidi upande wa mashitaka  mtuhumiwa alikutwa na hatia chini ya kifungu cha sheria f namba 130(1) na namba (2)(e) NA 131 sura ya 16 ya kanuni ya  adhabu.
Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi Hamimu Gwelo uliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 12 mwaka huu majira ya saa 8 mchana.
Aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine baada ya vitendo kama hivyo kukithiri  katika siku za hivi karibuni.
Mahakama hiyo ilipompa nafasi ya kujitetea mtuhumiwa aliomba mahakama isimpe adhabu kali kwa maana hilo ni kosa la kwanza kwake na anategewa na familia yake.
Baada ya utetezi huo mahakama iliamua kutoa hukumu ya kwenda jela miaka 30.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA