RAIS MAGUFULI AMETOA MSAADA MSIKITINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa msaada kwa Msikiti wa Noor Mkange, Miono, wilayani ya Chalinze mkoa Mkoa wa Pwani leo.
Waumini wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange,Miono,Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani,wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli kwa msaada wa zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili.
Zulia pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilayani Chalinze mkoa wa Pwani.
Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais Magufuli, amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo lililokusudiwa.
Sheikh Nassor mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo amesema,kwa niaba ya waumini wa Msikiti huo wamemshukuru Mhe.Rais kwa kuitikia ombi lao la kupata zulia na kwamba kwa kutimiza ahadi yake hiyo Mhe.Rais amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa watu asiyebagua dini wala kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.
Aidha Sheikh Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea kumuombea Mheshimiwa Rais na kuwataka watanzania wote nchinikuungana nao kumuombea Rais bila kujali itikadi za kisiasa ama imani za kidini kwani anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni kwa manufaa ya wananchi wote.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA