AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUBAKA MTOTO

Mahakama ya  wilaya ya Mpanda mkoani  Katavi imemuhukumu  Willson  John(34) mkazi wa  Kijiji cha Simbwesa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kutumikia jela kifungo cha  maisha  baada  ya kupatikana  na hatia ya kumbaka  mtoto (7)wakati akiwa anaoga bafuni.
Hukumu  hiyo ilitolewa jana  na hakimu mkazi mfawidhi  wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Chiganga  Tengwa baada ya kuridhika na  ushahidi  uliotolewa na upande wa  mashtaka.
Kabla ya kusoma hukumu  hiyo  hakimu  Tengwa alisema  mtu yoyote  anaefanya kitendo  kama  alichofanya mshitakiwa  huyo  anakuwa amefanya  kosa  kinyume  cha kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza  na 2E  cha  sheria namba 131 kidogo  cha  tatu  cha kanuni ya  adhabu.
Alieleza  kutokana  na  ushahidi  uliotolewa mahakamani na  upande  wa mashtaka uliotolewa  na  mashahidi sita  akiwemo  mtoto aliyebakwa  ambapo mshitakiwa  hakuwa  na  shahidi yoyote na mahakama  imeridhika  na  ushahidi huo wa upande wa mashtaka.
Hakimu Tengwa  alisema  miongoni mwa ushahidi uliomtia  mshitakiwa  hatiani  ni ule uliotolewa na mtoto mwenyewe aliyefanyiwa kitendo hicho pia daktari aliyemfanyia uchunguzi na kuthibitishwa kuingiliwa kwa  mtoto huyo kwenye  sehemu zake  za  siri na kuharibiwa hali  iliyomlazimu kumwanzishia dawa za kumkinga na maambuzi ya  VVU.
Pia ushahidi mwingine ni wa  mama  mzazi wa mtoto huyo ambaye aliutoa mahakamani kuwa mtoto wake alibakwa. 
Awali katika kesi hiyo mwanasheria wa Serikali  Fravian Shiyo alidai mahakamani hapo kuwa  mshitakiwa John  alitenda kosa  hilo Septemba 24 mwaka  huu majira ya saa 2:30 usiku nyumbani  kwao na  mtoto  huyo  ambako  mshitakiwa  alikuwa  amepanga  chumba  kwenye   nyumba yao wazazi wa mtoto aliyembaka  na wakati antenda kosa hilo wazazi wa mtoto huyo walikuwa wakiangalia  mpira  sebuleni kwenye TV.
 Alieleza siku ya  tukio  hilo mtoto  huyo   alikua amechukua maji kwaajiri ya kuingia bafuni kuoga  wakati alipokaribia  kwenye   mlango wa  bafuni alimkuta  mshitakiwa  akiwa  amesimama  karibu  na  mlango wa kuingilia  bafuni   na  ndipo  mshitakiwa  alipomtolea  kauli na kusema wewe  ingia tuu bafuni uoge  na  mie  nakuja  kupata  haja  ndogo  humo  humo.
Mwanasheria shiyo alisema  wakati  mtoto  huyo  akiwa anaendelea  kuoga  mshitakiwa  Willson aliingia ndani ya  bafu na  kumziba mdomo iliasipige kelele  mtoto  huyo  na kisha na  kisha  alianza  kumbaka na  alipomaliza  alimwachia  mtoto  huyo na  kumwambia  kuwa endapo angemwambia mtu  yeyote juu ya  kitendo   alichomfanyia atamuua.
 Aliendelea kuieleza mahakama hiyo aliyebakwa  awe  mwoga  na   asiwaambie  wazazi  wake  na  aliingia  ndani na  kumwomba  Mama  yake  ampatie  maji ya kunawa  hata   hivyo  mama  yake  alimkatalia  kumpa maji kwa kile  alichodai  mbona ametoka  kuoga  muda   si  mrefu maji ya  nini  tena.
Ndipo  mtoto  huyo alipoingia   ndani ya  chumba  alichokuwa   akilala   hata  hivyo  alishindwa kupata usingizi  kutokana na maumivu yalivyozidi   alimwagiza   mtoto mwezake wa  kike  amwite mama  yake  na  alipoingia  chumbani  alimkuta   akiwa  analilia  huku   godoro  alilokua   amelalialikiwa  limelowa  damu  na  ndipo  alipomtaja  mtuhumiwa  kuwa  ndio   aliyembaka.
Kabla ya kusomewa  hukumu  mshitakiwa  alipewa  ya nafasi ya  kujitetea  kama  anayosababu ya msingi ya  kuishawishi mahakama   imwone  hana  hatia au  impunguzie   adhabu.
 Katika  utetezi wake  mtuhumiwa alidai kuwa yeye hakutenda  kosa  hilo isipokuwa  ni  chuki za mama wa  mtoto  huyo ambaye  alikuwa amemwongezea  kodi ya  chumba  kutoka shilingi 20,000  hadi   40,000  ambazo  yeye  mshitakiwa  alikataa  kulipa  ongezeko  hilo.
Utetezi  huo  ulipingwa  vikali  na  mwendesha  mashitaka  wakili wa  Serikali  ambae   aliiomba  Mahakama  itowe   adhabu  kali  kwa  mshitakiwa  ili  iwe   fundisho  kwenye   jamii  kwa  watu  wenye  tabia  kama  hiyo .
Hakimu Ntengwa  baada  ya  kusikiliza  utetezi  huo  na  pingamizi  la upande  mashitaka  alisoma  hukumu na  kusema kuwa  mtuhumiwa   amahukumiwa  kutumikia  jela  kifungo cha  maisha yake  yoye  na  kama hajaridhika  na  uamuzi huo anayo nafasi ya kukata  rufaa  kwenye  mahakama ya juu ya  ngazi   nyingine na kisha alimpatia  nakala  ya  hukumu  hiyo na  kwenda  nayo gerezani.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA